Orodha ya ramani za nyumba zinazofaa kujengea nyumba ndogo Tanzania

Nini uhalisia wa nyumba ndogo?

Tunapokuja katika swala la ujenzi wa makazi ya kuishi familia, basi kuna mambo amabyo yamekuwa kama sheria ambayo yanaamua aina ya nyumba ambazo tunajenga. Baadhi ya mambo ni kama bajeti, tamaduni, majirani, hali ya hewa, staili… Kiujumla ktk jamii yetu tunapozungumzia nyumba ndogo tunamaanisha ni zile nyumba ambazo zinatumia nafasi ndogo ya kiwanja, zinazotumia bajeti ndogo, zilizo na urahisi kujenga n.k. Nyumba ndogo mara nyingi ni zile nyumba ambazo ukubwa wa sakafu wake upo chini ya mita za mraba 100 (sqm) na mara nyingi ni nyumba za vyumba 3 au viwili za kawaida (siyo ghorofa).

Hivyo kitaalamu nyumba ndogo ni zile nyumba ambazo zipo chini ya mita za mraba ~100 na zenye unafuu na urahisi kujenga. Maana hii inaweza badilika kutokana na mtu binafsi ambavyo anaweza kuamua. Maana hii pia inaangalizia zaidi jamii ya Kitanzania na Afrika Mashariki, hivyo kwa mtu ambaye yupo Ulaya anaweza kuta maana hii haikidhi sana.

Gharama za kujenga nyumba ndogo

Je, gharama za ujenzi za nyumba ndogo ni kiasi gani? Hili ni swali ambalo umekuwa ukihitaji kujibiwa. Kikawaida nyumba ya vyumba vitatu ya kawaida yenye ukubwa wa sakafu wa 120sqm kujenga Tanzania mpaka kuikamilisha finishing vyema ktk ubora mzuri itagharimu Tshs. ~50 – 65 Milioni, sasa tunapokuja nyumba ndogo inaweza gharimu kuanzia Tshs. 25 – 45 Milioni. Gharama hizi zinategemea sana na ukubwa haswa wa nyumba husika, staili na mtindo wa nyumba, idadi ya vyumba ktk jengo. Kujenga boma (msingi, kuta na paa) kwa nyumba hizi zinaweza kukugharimu kiasi cha Tshs. ~10 – 25 Mil kutegemeana na nyumba. Kwa Yule anayehitaji kujua gharama halisi kila nyumba ktk ramani zetu basi jiunge uanachama hapa ili uweze ona gharama kwa kila hatua ujenzi (msingi, kuta, paa, sakafu, dari, umeme…).

Sababu za watu kujenga nyumba ndogo

Zipo sababu nyingi ambazo zinaamua watu kujenga nyumba hizi ndogo na sasa tutaziangalia ili nawe uweze jihakiki kama kweli unahitaji kujenga nyumba hizi au huhitaji. Tutaangalizia pia na faida na hasara za kujenga nyumba ndogo.

  • Kuwa na bajeti ndogo kujenga

Watu wengi siku hizi wamekuwa wanataka kujenga nyumba ambazo zimejitoshereza kiuzuri lkn pia wataweza mudu gharama za ujenzi. Kutokana na kuwa na kiasi kidogo cha bajeti basi watu wengi wamekuwa wakiamua kujenga nyumba ambazo watamudu gharama lkn pia watazikamilisha vyema. Je, una Tshs. 15M na unataka kufanya ujenzi mzuri uliokamilika? Ndio inawezekana kwa kuanzia pesa hiyo kukamilisha boma la nyumba yako na ukahamia. Ijapokuwa pia ukijikita tuu kwenye gharama ndogo unaweza jikuta unaibana nyumba ikawa ndogo na ukapunguza uzuri, hivyo ni muhimu kubalance vyema bajeti na mahitaji yako. Fahamu zaidi gharama za ujenzi wa nyumba na namna ya kuokoa gharama ujenzi.

  • Eneo dogo la kiwanja

Viwanja ni gharama kununua haswa vile ambavyo vipo ktk maeneo muhimu na mazuri. Hivyo kama kiwanja chako ni kidogo na unapenda ujenge hapo basi unaweza jenga nyumba hizi ndogo vyema kabisa. Ni muhimu pia kuwa na uhalisia kama kiasi cha kiwanja hicho kitaweza kukutoshereza kwa shughuli zako zote unazotarajia ili uweze furahia nafasi yako. Fahamu zaidi aina ya kiwanja kinachofaa kununua.

  • Familia ya watu wachache

Zipo baadhi ya familia ambazo idadi ya watumiaji wa nyumba ni 3 tuu. Kuna wazee ambao wamestaafu, pia wale ambao wameamua kuishi bila kuoa aua kuolewa na labda wageni ambao unakuta wanataka nyumba ya kutosha watu wachache ambapo wanajikuta nyumba ambazo zinawafaa ni hizi za ramani ndogo. Hapa pia ni muhimu kuangalia kama idadi inaweza ongezeka au laa siku za mbeleni na kama nyumba itatosha.

  • Nyumba za kupangisha

Nyumba za kupangisha ni biashara nzuri na endelevu maana inakuletea kipato endelevu mara kwa mara kwa muda mrefu. Nyumba ya kupangisha ni uwekezaji hivyo inabidi ilete faida kwa muda wa haraka iwezekanavyo; Hivyo ni muhimu kujenga nyumba ya kupangisha ya vyumba 3 au 2 ndogo iliyojitoshereza na kutumia gharama ndogo kiujenzi ili kodi ambayo wateja watakuwa wanakulipa iweze rudisha haraka gharama yako ya ujenzi. Mtu aliyejenga nyumba kwa 30M atarudisha haraka gharama yake kuliko yule aliyetumia 50M na unaweza kuta kiasi cha pango kipo sawa. Ijapokuwa pia ni vizuri kuangalia ni aina ipi ya wateja wako unataka kuwapangisha ktk nyumba yako; je, ni wanaopenda nyumba kubwa au wanatosheka hata kwa nyumba ndogo?

  • Gharama ndogo za uendeshaji

Gharama za nyumba hazipo tuu ktk ujenzi, zipo pia ktk uendeshaji. Tunapozungumzia uendeshaji tunamaanisha kulipia gharama za usafi, matengenezo, kodi za serikali, umeme, maji, taka n.k. Hivyo kuna mwingine anataka gharama zake za kuendesha nyumba ziwe ndogo zaidi kwa kuchagua kujenga nyumba ndogo.

ID-
28694
2
84
sqm
34
Pcs
11
m
2,009
Pcs
8
m
745
Pcs
ID-
28439
2
64
sqm
59
Pcs
12
m
1,150
Pcs
5
m
572
Pcs
ID-
28222
2
107
sqm
44
Pcs
12
m
2,568
Pcs
12
m
952
Pcs
ID-
28041
2