Mambo 3 ambayo fundi unapaswa kuyamudu ili kukusaidia kupata kazi kwa urahisi zaidi.

TZ
From TZS 100,000/day
Kinondoni
10 years
I’m Engineer and developer to help you achieve your dream home for the welfare of your family!
Building Designing Cost Estimation Landscape Designing Building Setting Out House Building

Siku zote inahitajika ujuzi na makusudi ya dhati ili uweze kupata kazi au tenda za ujenzi kwa idadi ile unayoitaka. Kazi hutafutwa kwa maamuzi na sio kutegemea zije zenyewe bila jitihada. Ili upate kazi basi unapaswa ufanye kazi fulani ili uweze kupata kazi unayoitafuta. Unaweza ukawa na ujuzi na kipaji kizuri katika fani yako uliyonayo lakini pale ambapo fani yako haipati soko zuri basi hali hiyo inaweza kukukatisha tamaa na ukashuka moyo katika kuendelea kukua katika fani hiyo.

Ni muhimu kuweza kujifunza kanuni kadhaa ambazo zinaweza kukusaidia ili nawe uweze kumudu njia za kuweza kupata kazi kwa urahisi. Ujenzi ni taaluma na sio ubabaishaji nikiwa na maana ya kwamba unahitaji kuanzia sasa kuweka taratibu za kujifunza taaluma hii katika Nyanja mbalimbali zinazokuhusu. Yafuatayo ni mambo 3 kati ya mengi ambayo ukiyafuata yatakusaidia uweze kujua misingi muhimu ambayo itakusaidia uweze kupata kazi kwa urahisi kwa idadi unayokusudia.

Ubora

Swala la ubora ni muhimu kwanza kabisa kabla ya mambo mengine. Ubora tunaouzungumzia hapa ni ule unaohusu uimara wa kazi, finishing nzuri, mkono mzuri wa kazi, kiwango bora kinachotakiwa, kudumu kwa kazi, kupendeza kwa kazi, ubunifu katika kazi zako na ubora ule unaopitiliza matarajio ya mteja wako na akabaki anafurahia kazi uliyomfanyia. Swala la ubora ni pana sana.

Utawezaje kufanya hivi? Hapa ni papana kidogo lakini nitakuelezea kwa ufupi namna ya kuweza kufikia hatua hii.

Kwanza unapaswa ujue kazi gani ambayo unaipenda na ipo ndani yako; kwa lugha nyingine kipaji chako ni kipi? Wewe ni mzuri katika mambo ya aina gani? Unapenda kufanya kitu gani? Watu pia wamekuwa wakikusifia katika aina gani ya kazi? Unapaswa kuenea na kushamili katika kazi ile ambayo ni kipaji chako na ambayo unaipenda kuifanya. Ukiweza kufanya hivyo basi itakusaidia kutumia nguvu kidogo kuifanya kazi hiyo vyema sana lakini pia inakuwa ni rahisi kwako kujifunza mambo yanayohusu kazi yako kwa urahisi. Ukifanya hivi itakusaidia pia kuwa mvumbuzi na mbunifu katika kazi hiyo na uweze kushamili sana.

Nakubali kuwa mara nyingine katika majukumu na maisha mtu unajikuta unaifanya kazi ambayo sio kipaji chako au ambayo huipendi; lakini mwisho wa siku hakikisha unafanya kazi ile ambayo unaipenda; hakikisha kufanya kwako kazi kunakuwa kwa kupenda na unajivunia kwa kazi yako kuwa bora! Hakikisha kazi yako inabeba alama sahihi ya uzuri kuhusu wewe nikimaanisha kuwa kazi yako ni alama yako uliyoiacha. Hakikisha unajiwekea ratiba ya kujifunza na kujipanua kitaaluma katika kazi yako!

Network

Network ni neno la kiingereza ambalo lina maana ya mtandao. Kama mtaalamu unapaswa kujijengea mtandao imara wa kazi. Unapaswa uwe katika namna ambayo watu wanakufahamu unahusika na nini na unafanya nini haswa specifically. Unapaswa uwe katika sehemu ambayo pale kazi na fursa zinazohusiana na mambo ya ujenzi zinapokuja basi nawe zikupate (fursa za kazi huja mara nyingi katika mtandao wa kazi husika). Mtandao wako unapokuwa mkubwa basi chance yako ya kupata kazi nayo huwa kubwa. Mtandao wako unapokuwa umeenea maeneo mbalimbali, basi ni rahisi pia kwa wewe kuweza kupata kazi kutoka maeneo mbalimbali.

Zipo namna kadha za wewe kujenga mtandao utakaokusaidia kuweza kupata kazi zako kwa urahisi. Njia moja wapo ni kufahamiana na kujenga mahusiano mazuri na wale watu wenye maamuzi ya kazi fulani ifanyike ili siku wanapotoa maamuzi ya kazi fulani kufanyika basi na wewe uwepo katika mlolongo watakaoipata. Unaweza pia kujiunga na vikundi mbalimbali vya watu wanaofanya kazi za mtindo huo husika ili muweze kujuzana fursa na changamoto mbalimbali zinapotokea. Pia unashauriwa uwe na business cards za kuwaachia watu fulani muhimu ili wasikose mawasiliano na taarifa zako za kikazi.

Katika mtandao wetu wa Makazi tunaruhusu wataalamu mbalimbali wa mambo ya ujenzi kuweza kujisajiri bure na kuziweka taarifa zao za kazi za ujenzi mtandaoni ili mtu fulani anapotafuta mtaalamu wa aina fulani basi aweze kukupata. Ni muhimu kujisajiri katika mtandao huu kwa sababu miaka ya siku hizi yule ambaye hajajiunga na mfumo wa mtandao (internet) anakua mara nyingi amejitenga na fursa nyingi za kiuchumi. Ziweke mara kwa mara kila siku taarifa na kazi zako katika mtandao wako wa Makazi ili ikusaidie kuunganishwa na wateja kibao kutoka mikoa yote Tanzania na nje ya nchi.

Huduma kwa mteja

Huduma kwa mteja ni jambo la muhimu sana pale ambapo unataka kuwateka wateja. Wateja wanahitaji namna ya kuweza kuwamudu ili uweze kuendana nao. Bila kujali hali ya mteja na hadhi yake, mteja yeyote ni mfalme na chochote ambacho mteja anakisema au kukitaka hutakiwi kumkosoa bali unatakiwa ujue namna ya kuweza kumjibu na kumshauri vyema.

Kazi yeyote ambayo unaifanya ya mteja basi hakikisha umemkabidhi akiwa ameridhika na kuifurahia. Hakikisha mteja wako pale ambapo anafikiria kuhusu kazi fulani basi wewe uwe mtaalamu wa kwanza kukutafuta kwajili ya kazi hiyo. Mteja anapofanya kazi na wewe anapaswa ajisikie raha, usalama na kuridhika zaidi ya alivyotarajia.

Huduma kwa mteja haiishii katika kuifanya kazi tu, ila inakwenda hata baada ya kukabidhi kazi yako. Hakikisha unajijengea tabia na ratiba ya kutembelea kazi mbalimbali ambazo umeshawahi kuzifanya kwa wateja wako. Jitahidi uwe unajua mrejesho wa kazi ambazo umekabidhi miaka kadhaa iliyopita. Kwa zile kazi zilizopata hitirafu jitahidi kuangalia namna ya kufanya marekebisho kwa bure au ofa kama unaweza.

Kwa njia hii basi wateja wako watakuwa wamepata msaada mzuri katika mambo yao na wataweza kuwajulisha wengine kuhusiana na wewe. Siku zote binadamu hutafuta kwanza uhakika na usalama wa huduma au kitu fulani anachotaka kukinunua; uhakika na usalama hujengwa kwa kufahamiana na mahusiano mazuri. Hakikisha unajenga mahusiano mazuri ya kikazi na wateja wako yenye nidhamu na heshima na yasiyoleta nia ovu au kuleta mashaka kwa aina yeyote. Hakikisha pia unahifadhi mawasiliano ya wateja wako vyema siku zote.

Kama ambavyo nimeeleza kwa ufupi kuhusu namna ya kufanya ili uweze kupata kazi nyingi kwa urahisi zaidi, basi ni muhimu kuhakikisha unachukua hatua zaidi katika kujifanya bora katika kazi zako. Siku zote akili yako inapaswa kujikita katika kuhakikisha unampatia mteja wako kitu ambacho kitamfurahisha zaidi ya alivyofikiria. Hiyo iende sambamba na kuweka juhudi katika mtandao wa kupata kazi ili ajira yako iwe yenye tija na usikatishwe na tamaa. Jiunge sasakatika mtandao wa Makazi kama njia mojawapo ya kujiongezea network ya kazi kutoka mikoa yote Tanzania na nje ya nchi.

Tupe maoni yako hapa chini namna mtandao inavyokusaidia kupata kazi!

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TZ
From TZS 100,000/day
Kinondoni
10 years
I’m Engineer and developer to help you achieve your dream home for the welfare of your family!
Building Designing Cost Estimation Landscape Designing Building Setting Out House Building
ID-15044
3
163 sqm
132 Pcs
15 m
2,918 Pcs
15 m
1,451 Pcs
ID-14855
3
160 sqm
75 Pcs
15 m
2,923 Pcs
14 m
1,642 Pcs
ID-17219
3
148 sqm
102 Pcs
13 m
2,653 Pcs
13 m
1,319 Pcs
ID-27834
4
280 sqm
57 Pcs
13 m
8,686 Pcs
13 m
2,165 Pcs
ID-21652
4
301 sqm
124 Pcs
14 m
6,520 Pcs
12 m
2,146 Pcs
ID-15336
5
440 sqm
125 Pcs
19 m
8,921 Pcs
16 m
2,266 Pcs
ID-18140
2
382 sqm
123 Pcs
17 m
9,487 Pcs
12 m
2,726 Pcs
ID-16416
4
210 sqm
95 Pcs
16 m
5,005 Pcs
13 m
1,869 Pcs
ID-17182
4
220 sqm
78 Pcs
15 m
6,027 Pcs
10 m
1,400 Pcs
ID-16941
3
167 sqm
115 Pcs
15 m
2,989 Pcs
13 m
1,486 Pcs
ID-14910
2
269 sqm
58 Pcs
16 m
5,596 Pcs
14 m
1,450 Pcs
ID-19158
1
212 sqm
87 Pcs
18 m
5,085 Pcs
14 m
1,886 Pcs
Apr 2024
Marekebisho ya paa kuvuja la hidden roof (contemporary) maeneo ya Kimara Korogwe, tatizo mwinuko mdogo wa bati
building_inspector roofing Waterproofing
Ubungo, TZ
TZS 5 Mil
Feb 2024
Designing na Kusimamia ujenzi wa nyumba ya kupangisha na maduka aina ya Contemporary
architectural construction_manager
Ubungo, TZ
TZS 110 Mil
TZ
From TZS 40,000/day
Kinondoni
23 years
Mtaalamu wa kujenga na kurekebisha mapaa ya nyumba mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 23, anayepatikana Tanzania. Anajulikana kwa ustadi wake katika ujenzi wa mapaa ya nyumba, kupiga dari, pamoja na uwekaji kuta na mapambo ya gypsum. Ally amekuwa akitoa huduma kwa uaminifu mkubwa na amepata mafunzo maalum katika kuweka vigae vya Decra, hivyo kuhakikisha ubora katika kazi zake.
Brandering Ceiling Gypsum Decoration Sheet Roofing Gutter Installation Shingle Roofing Tile Roofing Timber Trussing
TZ
From TZS 75,000/day
Ubungo
9 years
An accomplished designer, Quantity Surveyor, and builder based in Dar es Salaam, Tanzania, specializing in residential construction. With a background in designing and quantity surveying, he brings a wealth of expertise to crafting bespoke homes that seamlessly blend functionality with aesthetic appeal. His commitment to quality craftsmanship and innovative design solutions has earned him recognition in the industry. From modern villas to traditional residences, he excels in delivering projects that exceed client expectations and elevate living spaces
architectural construction_manager fencing foundation_repair framing guttering project_manager quantity_surveyor repairs roofing Welding
TZ
From TZS 50,000/day
Ubungo
10 years
Mtaalamu mzoefu katika ujenzi nyumba, haswa ktk ufundi uashi na ujenzi matofali, aliyehitimu kutoka Chuo cha Ufundi Arusha. Tangu utotoni, alifundishwa na familia yake, ambao pia wanahusika katika ujenzi wa makazi. Akiwa Ubungo, Tanzania, Charles anafanikiwa katika ujenzi wa makazi kwa ujumla, akitoa ubora na uimara katika kila mradi. Ujuzi wake unajumuisha uwekaji wa matofali, kazi za zege, uwekaji wa sakafu, upakaji wa plasta, mabomba, paa, na zaidi, kuhakikisha utoaji wa huduma kamili. Charles anaunganisha uzoefu wa vitendo na mafunzo rasmi, akiwa na dhamira ya kutoa ubora katika ujenzi wa makazi kote Tanzania.
Bricklaying concrete_work construction_manager Flooring Masonry Plastering Plumbing roofing septic_systems Tiling