Usanifu wa Mandhari ya nje au Landscape Design

Utengenezaji wa mandhari (Landscaping) ni utengenezaji wa mazingira yanayozunguka majengo na makazi ya binadamu ili yawe yenye kukidhi matumizi na yenye kuleta uzuri, mvuto, afya na ustawi wa jamii huku yakizingatia uhifadhi wa mazingira. Utengenezaji huu huusisha kubadili na kuboresha sura na kontua za ardhi, uboreshaji miti na mimea, kuweka vitu na samani katika mandhari husika katika utaalamu maalum. Baadhi ya shughuli ambazo zinahusiana na Utengenezaji mandhari ni bustani na viwanja vya mapumziko, vibanda vya mapumziko, migahawa ya bustanini, sebure za bustanini, majiko ya nje ya nyumba, maeneo ya michezo, mabwawa ya kuogelea, mashimo ya kuotea moto, maeneo ya kuchomea nyama, nyua na vibaraza, sitaha, sehemu za maegesho ya magari, njia za kupita, nyumba za vivuli, wigo, taa za nje, Kamba za kuanikia nguo, malango, majabari, vilima vya udongo, madimbwi, mifereji, nyumba za kuoteshea mimea, mifumo ya umwagiliaji maji, uvunaji wa maji ya mvua, visima, chemchemi, maporomoko ya maji, upandaji wa miti na mimea n.k. Utengenezaji huu huanza katika hatua ya kwanza ya kusanifu mazingira kitaalamu kwa kufuata taaluma husika kisha huingia katika hatua ya kujenga mandhari hayo kulingana na michoro na maelezo ya kitaalamu. Ujenzi wa mandhari hufanyika kwa umakini na utaalamu ili kufanikisha kuweka mazingira katika mvuto mzuri. Wataalamu mbalimbali huusika ili kuleta kazi iliyo katika ubora wake; wahandisi, wasanifu mandhari, wataalamu wa mimea, wataalamu wa umeme na maji n.k. Ila kwa sasa hapa tunakupa huduma ya landscape design.

[wpsm_toggle title=”Lipia ada ya huduma hii au Piga +255-657-685-268″] [super_form id=”13776″] [/wpsm_toggle]

Project 1     Project 2

Makazi Icon Blue

Join Membership

Join Membership to See Clear Floor Plans Before You Buy the Full Plan; See How Much MONEY is Needed to INVEST in Your Business In order to Get the Profit to Finance Construction of This House. What MORTGAGE to Borrow and Return Monthly to Your Bank. Also, See How Much it COSTS to Build the Foundation, Walling, Roofing, Ceiling, Painting, Doors, Windows… in All of Our Houses on This Platform so That You Can CHOOSE, COMPARE, PLAN & STRATEGIES on How to Approach Your Construction Rightly!