Gharama za ujenzi wa nyumba yako

Hapa tunachambua kuhusu gharama za ujenzi wa nyumba yako! Je, gharama hizi zinatoka wapi? Kwanini zifike hapo? Vipengere gani vya ujenzi vinaunda hizo gharama? Mgawanyiko wa hizo gharama upoje kwa kila steji ya ujenzi? Njia rahisi ya kufanya makadirio ya gharama ya ujenzi. Kumbuka hapa tunazungumzia kuhusu nyumba ya kuishi familia. Hapa utaweza kupata mwanga utakaokusaidia kucheza na uchumi wa ujenzi na uweze kuokoa gharama na pia mada hii itakupa ujasiri wa kujitoa kulipa gharama stahiki za ujenzi wako!

Kwanza gharama za nyumba ni thamani ambayo unapaswa kuilipa ili uweze kuipata nyumba hiyo unayoitaka! Sasa thamani unaweza ilipa kwa njia ya pesa, nguvu kazi yako, nguvu ya akili na pesa. Ina maana bila kulipa gharama stahiki huwezi pata thamani ya nyumba ile unayoitaka. Gharama hizi unaweza walipa watu wengine wanaokufanyia kazi au wanaokuuzia bidhaa, lakini pia waweza zilipa wewe mwenyewe kama muda na nguvu zako. Bila kulipa gharama stahiki huwezi pata nyumba hiyo.

Kiujumla gharama za ujenzi wa nyumba haswa zinajumuisha gharama za VIFAA + UFUNDI

  • Vifaa inajumuisha vitu kama mchanga, saruji, vyuma, nondo, milango, madirisha mawe n.k.
    • wastani wa gharama ya vifaa katika ujenzi wa nyumba ni ~70% ambapo ndio huchukua kiasi kikubwa cha gharama. Kumbuka vifaa ambavyo inabidi vitumike ktk ujenzi vina kiwango stahiki cha kitaalamu hivyo ukisema utumie vifaa duni au feki au visivyotakiwa basi utapata nyumba ambayo haipo sawa na inaweza leta madhara na hasara zaidi.
    • Ni muhiu kujua viwango vya vifaa vya ujenzi ambavyo vinatakiwa ktk kujenga nyumba yako kutoka kwa wataalamu wa ujenzi haswa msanifu na mhandisi wako.
    • utumizi wa vifaa kipindi cha ujenzi nao unatakiwa ufanyike vyema kwa kiwango ili kuhakikisha kile kinachotakiwa kitokee kinatokea
  • Ufundi ni muhimu sana katika kufanikisha nyumba yako maana ndio injini ya ujenzi wako.
    • Ufundi huchukua wastani wa ~30% ya gharama nzima ya ujenzi wako.
    • Ufundi ndio unaovitumia vifaa na kuvifanya viwe nyumba. Ufundi ni taratibu, ustadi na kipaji kitakacho kusaidia kupata nyumba yenye ladha na uimara unaotakiwa.
    • Ufundi mbaya unaleta nyumba mbovu na pia unaweza leta hasara ktk ujenzi wako. Hakikisha unatumia wataalamu wenye stadi stahiki ili uweze kuvibadili vifaa vyako kuwa nyumba inayotakiwa ya ndoto yako.
    • Mlipe fundi wako vyema ili aweze fanya kazi kwa moyo na kumpa motisha zaidi na aachilie kipaji chake kwa hali ya juu zaidi

Leo tutazungumzia haswa gharama za ujenzi kwa nyumba ya kuishi familia ya kawaida. Swala la ghorofa litadokezwa kidogo tuu.

 

Ghorofa kwa ufupi
  • Ghorofa lina gharama zake na kama tulivyo discuss siku za nyuma tuliona gharama ya ghorofa inaweza kwenda ifuatavyo kama muongozo wa haraka (kujenga mpaka kufanya finishing, vyumba 4, ghorofa moja)
    • Ghorofa za gharama nafuuu huweza kwenda gharama Tsh. 100M – 150. Waweza tazama mfano wake huu na huu mwingine.
    • Ghorofa la kawaida linakwenda gharama around Tsh. 180M – 250M
    • Ghorofa premium special linaweza kwenda around Tsh. 350M na kuendelea. Mfano kama hili hapa.
    • kwa hiyo unavyojenga ghorofa lako inapaswa uwe umejipima na kukubali gharama ili ujenge inavyotakiwa na ubora stahiki.

 

Nyumba ya kawaida
  • Nyumba ya kawaida ambayo ndio tutazungumzia zaidi zinakwenda kutoka wastani Tsh. 25 – 125M kwa vyumba 3 ya kuishi familia kutegemeana na wewe mwenyewe utakavyoamua staili, ukubwa na kiwango cha finishing
    • kwa vyumba 3 muongozo wa gharama
      • nyumba za gharama nafuu zinaweza kuwa na ukubwa wa mita za mraba ~90sqm, gharama ya kujenga Tsh. 25 – 40M. Mfano hizi.
      • nyumba za kawaida vyumba 3 au 4 zinaweza kwenda around Tsh. 50M – 70M. Mifano yake hii ukitoa maghorofa hayo.
      • nyumba bungalow zinaweza kwenda around Tsh. 90 – 125M. Mifano yake hii na hii nyingine.

 

  • Mara nyingi gharama za ujenzi kwa haraka hupimwa kwa kuangalia ukubwa wa mita mraba za sakafu za jengo ; jengo kubwa ndilo lenye gharama kubwa. Hivyo kama unataka jengo lako lisiwe na gharama kubwa sana basi ni vyema kuangalia namna ya kupunguza ukubwa wa jengo.
    • Mfano wa kupima ukubwa nyumba yako (eneo la sakafu la nyumba yako) ikijumuisha korido, vyumba, vibaraza (eneo lote ambalo lipo ndani ya msingi wa nyumba yako)
      • nyumba hiyo ya juu ina jumla ya mita mraba za ukubwa wa 6SQM + 12SQM +24SQM = 42SQM
      • Kikawaida kwa Tanzania kila mita moja ya mraba (1 SQM) inagharimu Tsh.~ 500,000/= za bei kujenga kila kitu mpaka finishing nyumba ya bati ya tofali. Kiwango hicho cha 500,000 hutegemeana na eneo, staili, ukubwa wa nyumba… ila kwa makadirio tunatumia Tsh. 500,000/=
      • Hivyo gharama ya kujenga kwa nyumba hiyo ya hapo juu ni Tsh. 500,000 x 42 = Tsh. 21,000,000/=
        • huu ni wastani tukifanya assumption kwamba umejenga vyema ktk kiwango bora cha kihandisi bila kuchakachua na umepiga paa la bati.
        • Tumia KIKOKOTOZI HIKI RAHISI KUJUA GHARAMA ZA NYUMBA YAKO KWA KUTEGEMEA UKUBWA WA NYUMBA

 

  •  Mchanganuo wa gharama za ujenzi wa nyumba ya kawaida nao twaweza kuupata kama jedwari hili hapa chini linavyoonesha
    • Ufafanuzi wake zaidi
      • ukiangalia hapo juu PAA ndio inachukua ~16% kama kiasi kikubwa cha gharama kuliko vitu vyote ktk ujenzi
        • kwa Dar es Salaam mbao ndio hula gharama zaidi ikifuatiwa na bati na gharama ya kumlipa fundi
      • Kitu cha pili ni MSINGI ndio unakula ~12%
        • gharama za kuchimba msingi, zege la chini kabla ya kupanga tofali, mawe yanayotandikwa juu, zege la jamvi, kushindilia, karatasi la kuzuia unyevu, dawa ya wadudu, nondo, formwork na vingine vingi ndivyo vinakula gharama zaidi.
        • kila kitu ktk msingi kina kazi yake. Kupunguza kifaa fulani hupunguza ubora fulani wa nyumba. Kutoweka karatasi la unyevu linaweza sababisha kuta na sakafu yako ikawa na unyevu nyevu. Kutoweka mawe ktk msingi huweza pelekea unyevunyevu ktk sakafu na kuta; na pia huweza sababisha sakafu kutokuwa imara.
      • Ukiweka Madirisha ya Aluminium au PVC au Mbao ngumu basi gharama nayo inakuwa kubwa ya madirisha
      • Kuta ikiwa maana ya tofali na plasta hula ~8% ya gharama
      • Msingi + kuta + zege + paa hula jumla ya ~44% ya gharama nzima ya ujenzi. Msingi, kuta, zege na paa ndivyo vinavyounda nyumba kuu (boma) na kwa kweli unaweza hamia. vitu vingine vilivyobaki ~56% ni mambo ya finishing.
        • utagundua nyumba yenyewe ni 44% tuu lakini mambo ya urembo na ladha yanakula ~56% ya gharama zako za ujenzi
        • ni muhimu kuhakikisha Boma (msingi, kuta, zege, paa) vinajengwa ktk ubora kabisa maana hii ndio nyumba yenyewe, kurekebisha vityu hivi vikiwa tayari vimeshajengwa ni gharama sana. Mambo ya finishing waweza rekebisha kwa urahisi kama kupaka rangi, kubadili taa…
        • wawezahamia nyumba yako ukiwa umefika mpaka e ya kupiga paa halafu vingine ukawa unavifanya huku umehamia ktk nyumba yako
        • Rangi zinafafanua hiyo steji unaweza ukawa unafanya nini ktk ujenzi wako
        • Kwa hiyo swala la gharama unavyojenga unaliendea pole pole kwa steji.
    • Tumia KIKOKOTOZI HIKI KUJUA GHARAMA YA KUJENGA NYUMBA YAKO KWA KILA STEJI kwa kutegemea ukubwa wa nyumba.

Waweza uliza swala lako hapa chini ujibiwe zaidi

15 responses

  1. YOUR DOING A GREAT JOB. KINDLY ASKING FOR MORE HOUSE MAP SAMPLES ESPECIALLY FOR TWO ROOMS KIND OF HOUSES WITH CLASSICAL ROOF DESIGNS

      1. Kiukweli nimependa elimu yenu natumai nitajiandaa vyema kabla ya kuanza kujengaa

  2. Habari za wakati huu nataka kuamua kujenga sasa lakin nataka nyumba simple thu ya vyumba viwili kimoja self na kingne kawaida

    1. Ivi gharama ya ujenzi kuanzia tofari mpka finishing mpka kilaktu yan sijui nondo madrisha malumalu cjui gharama nzima nyumba yenye viumba vitano ya kulala uku ikiwa na daining room pia ni shingap

    1. Tumia mafundi local kwa namna hii
      – angalia ubora wa kazi zake ambazo amewahi kuzifanya na uridhike
      – fundi awe na nidhamu ya kazi yake na kipenda kazi
      – ajikite ktk ubora wa kazi zaidi
      – ajue kusoma ramani
      – mhakiki kama anaweza kujenga hicho kinachotakiwa

  3. Ahsante kwa maelekezo yenu mazuri. Natumai kandri ya mda unavoenda ntajifunza kitu kuhusu gharama za ujenzi wa nyumba Bora.

  4. Am delighted with your great work, am a third year studented pursuing my civil eng. Studies at MBEYA UNIVERSITY OF SCIENCE AND TECHNOLOGY,am interested to work with you so as to gain competence and real exprrience of my career. Where can I get you. Am from Tanzania. Thanks

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ID-19205
3
130 sqm
53 Pcs
14 m
3,120 Pcs
12 m
1,157 Pcs
ID-16381
4
187 sqm
129 Pcs
17 m
3,367 Pcs
14 m
1,665 Pcs
ID-18569
5
232 sqm
135 Pcs
19 m
4,253 Pcs
14 m
1,751 Pcs
ID-15127
3
202 sqm
93 Pcs
18 m
3,616 Pcs
15 m
1,798 Pcs
ID-19705
2
61 sqm
56 Pcs
12 m
1,092 Pcs
6 m
543 Pcs
ID-16337
2
128 sqm
95 Pcs
14 m
2,291 Pcs
11 m
1,139 Pcs
ID-28462
4
230 sqm
192 Pcs
19 m
4,112 Pcs
15 m
2,044 Pcs
ID-17679
3
212 sqm
88 Pcs
14 m
6,086 Pcs
13 m
2,630 Pcs
ID-15801
3
117 sqm
64 Pcs
13 m
2,094 Pcs
12 m
1,041 Pcs
ID-17204
4
223 sqm
153 Pcs
19 m
4,023 Pcs
17 m
1,985 Pcs
ID-15044
3
163 sqm
132 Pcs
15 m
2,918 Pcs
15 m
1,451 Pcs
ID-26540
4
215 sqm
148 Pcs
17 m
3,849 Pcs
16 m
1,914 Pcs
Makazi Icon Blue

Join Membership

Join Membership to See Clear Floor Plans Before You Buy the Full Plan; See How Much MONEY is Needed to INVEST in Your Business In order to Get the Profit to Finance Construction of This House. What MORTGAGE to Borrow and Return Monthly to Your Bank. Also, See How Much it COSTS to Build the Foundation, Walling, Roofing, Ceiling, Painting, Doors, Windows… in All of Our Houses on This Platform so That You Can CHOOSE, COMPARE, PLAN & STRATEGIES on How to Approach Your Construction Rightly!

Eng. Lwifunyo Mangula
Payment Challenges? WhatsApp Admin