JE, NI AINA GANI YA KIWANJA KINAFAA KUNUNUA?

TZ
From TZS 100,000/day
Kinondoni
10 years
Mtaalamu wa mambo ya ujenzi wa makazi aliyesomea na mwenye uzoefu wa muda mrefu, kutoka kwenye kusanifu ramani za nyumba, usanifu wa nadharia ya nje ya nyumba na bustani, pamoja na mambo ya makisio na mahesabu ya gharama za ujenzi. Lengo letu ni kukuwezesha kutimiza nyumba ya ndoto yako sasa, bila kujalisha kama ni ya gharama nafuu au mjengo wa heshima.
3D Rendering Building Designing Cost Estimation Landscape Designing Project Management Project Planning Technical Drafting

TAMBUA MAHITAJI YAKO

Ni jambo la msingi kwanza kutambua unanunua ardhi kwajili ya kufanyia shughuli gani; je, ni makazi, biashara, huduma za jamii, viwanda n.k. Hii ni hatua ya awali kabisa kwani itakusaidia kuweza kuamua majibu ya maswali mbalimbali utakayo kutana nayo mbeleni. Ni muhimu kuchanganua uhitaji wako wa ardhi katika matumizi utakayofanyia, mipango ya muda mfupi na mrefu, nani atakayekuwa anaitumia ardhi hiyo.

Kuna sheria mbalimbali ambazo zimewekwa kuhusiana na ardhi na matumizi yake. Sheria hizi zinambana mtumiaji wa ardhi kutokana na shughuli fulani. Mfano, kuna maeneo ambayo hayatakiwi kuendeleza makazi ya watu ila shughuli za umma zinaruhusiwa; kuna maeneo ambayo ni maalumu kwa ajili ya viwanda, makanisa, michezo n.k. Kujua uhitaji wako ni muhimu ili uweza kununua ardhi itakayokidhi mahitaji yako ya sasa na ya muda mrefu.

Ni muhimu kujua kitu unachotaka kufanya kitahitaji ardhi yenye tabia gani za muhimu? Na pia kitu hicho kinahitaji ardhi isiwe na tabia gani? Mfano, unataka kujenga nyumba ambayo unataka iwe na shamba la mifugo; swali la kujiuliza, je, mifugo hiyo itakuwa ya aina gani na ni mingapi? Je inaruhusiwa kufuga nyumbani? Unataka kujenga nyumba ambayo itakuwa na uwanja wa mpira wa miguu; swali la kujiuliza, je, ukubwa wa uwanja utakuwa kiasi gani? Unataka kujenga ukumbi wa harusi; swali la kujiuliza, je, unataka ukumbi uwe wa kuchukua watu wangapi? Unataka kujenga shule; swali la kujiuliza, je, usalama na utulivu kiasi gani utauhitaji?

Jiulize maswali haya; vitu gani ambavyo umepanga kuvifanya baadaye ambavyo vitahitaji uwe na ardhi? Kisha chambua kila kitu kinahitaji ardhi yenye tabia gani za muhimu. Pia chambua kila kitu kinahitaji ardhi ambayo haina nini?

NUNUA ARDHI YENYE UKUBWA UTAKAOKUTOSHA

Swala la ukubwa wa ardhi lipo katika kipengere cha kwanza; tutalichambua zaidi kwani watu wengi wamekuwa wakipata shida hapo. Ukubwa unaofaa wa eneo unatokana na matumizi yaliyokusudiwa. Tukiangalia kwa undani katika makazi ya watu, kuna vitu vya muhimu ambavyo ni lazima viwepo katika makazi mfano choo. Vitu vingine vina umuhimu kutokana na mahitaji ya mtumiaji japo si lazima. Ni muhimu kutambua mahitaji yako ili kujua ukubwa kiasi gani unahitajika. Zipo sheria ambazo zinaongoza matumizi ya eneo na ukubwa wake unaohitajika.

Napendekeza yangu, kama unataka ardhi kwajili ya kujenga nyumba ya kuishi ya vyumba vitatu angalau upate mita za mraba 400 au zaidi; na kama unataka iwe na eneo la michezo, bustani, magari n.k. Basi angalau mita za mraba 500 au zaidi. Kama unataka kujenga nyumba ya ndoto yako yenye vyumba vyote vya muhimu na maeneo ya kupumzika nje basi angalau upate mita za mraba 900 au zaidi. Wataalamu wa kusanifu majengo na mabwana ardhi wataweza kukusaidia kuhusiana na ukubwa wa ardhi utakao hitaji.

Kuna baadhi ya watu wamekuwa wakijenga nyumba ambayo imebanana hata eneo la kupita ni shida. Wapo wengine wamejenga nyumba za kifahari za mamia milioni katika viwanja ambavyo hata gari halitoshi kuwekwa. Thamani ya jengo inaweza kukinzana na hadhi ya kiwanja! Swala la maeneo ya nje ya nyumba ya kupumzika na bustani ni muhimu kwa hali, ustawi na afya njema kwa binadamu; jitahidi kuyajumuisha kwenye nyumba yako.

FANYA MAAMUZI MAZURI KUHUSU GHARAMA

Swala zima la gharama ni muhimu kulitazama. Bei ya ardhi inatofautina kutoka eneo, matumizi, muda n.k. Ni muhimu kununua ardhi ambayo utaweza kumudu gharama. Ni gharama za sasa na za baadaye. Pia nunua ardhi ambayo itaweza kuuzika.

Swala la bei ni muhimu kulitafakari vizuri; kuna watu ambao wamenunua ardhi ambayo haiwafai kwaΒ  matumizi yao, sababu iliyowasukuma tu kununua ni bei ndogo. Nunua ardhi ambayo inaendana na matumizi yako. Itakuwa hasara kujenga jengo la biashara lenye gharama kubwa katika eneo ambalo wateja hawawezi kufika. Au umejenga ghorofa la milioni 200 katika kiwanja ambacho hata sehemu ya kupaki gari haipo. Changanua thamani ya mradi unaotaka kuuweka katika ardhi hiyo na bei ya ardhi hiyo. Je, ardhi hiyo inarutubisha mradi wako? Ikiwezekana lipia gharama hata kama ni kubwa ili tu upate ardhi itakayo kufaa.

Pia kuna gharama nyingine za pili ambazo vinahusiana na ardhi yako, mfano gharama za usafiri, gharama za ujenzi, gharama za vyakula na mahitaji mengine ya kibinadamu. Inawezekana sehemu ambayo unataka kununua ardhi ina gharama za maisha kubwa mno au gharama za usafili kutoka eneo hilo mpaka sehemu ya kupata huduma za jamii ni kubwa. Ni muhimu kuchanganua hayo mambo na kuyapatia maamuzi yanayofaa.

Swala la kununua ardhi ambayo itaweza kuuzika siku za mbeleni ni muhimu kwani linaweza kuashirilia thamani ya ardhi yako. Swali la kujiuliza je, siku ukitaka kuiuza utapata wateja? Je itaweza kuuzika kwa gharama ya juu zaidi ya uliyonunulia? Hii itaashiria thamani, hatari na hasara ya eneo lako!

Jambo la msingi ni kununua ardhi inayokufaa kwa bei nafuu. Kununua ardhi kwa bei ndogo siyo sawa kama ardhi hiyo haikufaii. Ni muhimu kununua ardhi yenye ukubwa, tabia ambazo zitaweza kukidhi mahitaji yako. Pia kuwa makini na mfumo unaotumia kununua ardhi yako; tumia mfumo wenye uhakika na wenye gharama nafuu!

TAMADUNI ZA ENEO

Tamaduni na uhali wa eneo ni muhimu katika kuchagua kiwanja kitakachokufaa kwa kuishi! Taratibu na kanuni za maisha za maeneo mbalimbali hutofautiana kwa sana. Inawezekana taratibu na kanuni hazijaandikwa katika maandishi na vitabu, bali namna mazoea ya eneo hilo huweza kuwa kama kanuni. Kuna baadhi ya mambo ukifanya katika jamii fulani unaweza kuhojiwa kwa nini umeyafanya. Taratibu za kila siku za kazi, usafi, uongozi, dini, sherehe na mijumuiko ya kijamii huchangia katika kuathiri utamaduni wa sehemu. Ni muhimu kuwa makini katika kuchagua tamaduni ambayo itakufaa na kwa ajili ya faida yenu!

Mitazamo ya watu wa maeneo fulani ni msingi wa namna ambavyo wanavyoendesha maisha. Kuna baadhi ya maeneo mtazamo wao ni uovu, kushindwa, ugomvi, uvivu, uchafu n.k. Mtazamo ndio unaokuongoza namna ya kutatua changamoto za kila siku! Ni muhimu kuweza kuchagua sehemu yenye manufaa kiroho, kiakili na kimwili. Sehemu utakayoishi itakuwa na mchango katika namna ambavyo maisha yako ya kila siku yatakavyokwenda. Marafiki, uongozi, majirani, mifumo ya biashara, misimamo, uchumi, usafi n.k wa eneo hukuathiri namna maisha yako yatakavyokuwa. Pia hata wewe kuwepo eneo fulani huathiri namna maisha ya eneo hilo yanavyokwenda.

FUATA TARATIBU ZA KISHERIA, HUSISHA SERIKALI

Kufuata taratibu za kisheria ni muhimu kwasababu hizi ndizo zinazokupa mamlaka na uhalali. Japo watu wengi wamekuwa wakinunua viwanja kienyeji na kujenga kienyeji, wapo baadhi yao wameishia kuingia katika migogoro na hasara za hata mamilioni. Kwa kipindi hiki hatuna budi kubadilika na kuanza kufuata taratibu husika ili tufanye uwekezaji wenye uhakika. Ardhi ni mali ya serikali; hivyo ni muhimu kuihusisha ngazi husika ya serikali. Taratibu za kisheria zinaweza kukusaidia kujua maeneo yenye migogoro, maeneo ambayo hayaruhusiwi kwa makazi n.k.

Kwa kukudokeza kidogo ni muhimu kufanya mikataba ya kimaandishi, kuhakikisha eneo hilo limaruhusiwa kisheria kwa shughuli unayotaka kufanya, kutambua uhalali wa anayekuuzia, kuhakikisha hakuna mgogoro, bei, anwani, picha, sahihi zenu ziandikwe, mipaka ya kiwanja ioneshwe, hadhi ya kiwanja kuhusu kodi ioneshwe n.k. Hayo ni baadhi ya mambo kuhusu sheria naΒ  inapaswa kuyajua zaidi kwa undani. Hapa pia linakuja swala la muhimu la kumhusisha mwanasheria aliyebobea katika mambo ya ardhi ili awape msaada wa kitaalamu wa kisheria kwani wengi wetu hutuzijui sheria vizuri.

Swala la kuhusisha serikali ni muhimu kwani ardhi ni mali ya serikali. Uhusishaji wa serikali katika manunuzi itakusaidia kujua hali ya hilo eneo kijiografia, uhalali wa eneo, mipango ya kiserikali kwa maeneo hayo, sheria kuhusu maeneo hayo n.k. Ngazi ya serikali inayoweza kukusaidia kwa haya ni halmashauri ya manispaa husika kitengo cha ardhi na sio kwa serikali ya mtaa. Epuka kutozwa gharama zisizo eleweka, kwani nitategemea malipo halali yote yafanyike kwa risiti halali ya halmshauri ya manispaa na si kwa serikali ya mtaa.

HALI YA HEWA NA YA UDONGO YA ENEO

Hali ya hewa hujumuisha joto, baridi, mvua, upepo n.k. Vitu hivi huathiri majengo, mimea, binadamu na wanyama! Hali ya hewa huweza kuathiri afya ya binadamu ambao wanatumia eneo hilo. Ni muhimu kuchagua eneo lenye hali ya hewa ambayo inafaa kwa watumiaji. Kuna baadhi ya magonjwa huwa na athari kubwa kutegemeana na hali ya hewa; sasa ni muhimu kujua uhusiano wa afya zenu na hali ya hewa kabla ya kuchagua eneo la kiwanja. Pia inawezekana kuna baadhi ya shughuli za kiuchumi za binadamu zinategemea hali ya hewa, mfano kilimo, ufugaji n.k. Basi jaribu kuchanganua namna ambavyo shughuli zako za kiuchumi zinavyoathiliwa na hali ya hewa kisha tambua ni hali ya hewa zipi zinafaa na ambazo hazifai.

Hali ya udongo ni muhimu kuliangalia kwa jicho la pana. Udongoni ndipo ambapo jengo, mimea hukaa. Hali ya udongo inaweza kuwa yenye rutuba, tindikali, tope, kichanga, mfinyanzi, mawe, mwamba, sumu, unururishi, mmomonyoko n.k. Hizi hali zinaathiri mimea, wakazi, gharama za ujenzi n.k. Japo mambo haya ni ya kitaalamu zaidi, lakini bado ni muhimu kuyatambua.

Eneo lenye udongo mfinyanzi linaweza kusababisha gharama za ujenzi wa msingi liongezeke hata zaidi ya mara mbili. Udongo mfinyanzi hutanuka unapopata majimaji na husinyaa unapokauka, hali hii hufanya jengo kunyanyuliwa na kushushwa; hii huweza kusababisha utokeaji wa nyufa katika jengo na kulifanya lisiwe imara. Inapowezekana kuepuka eneo lenye udongo mfinyanzi ni muhimu kufanya hivyo. Kama itakuwa vigumu kuepuka eneo lenye udongo mfinyanzi basi ukubaliane kulipia gharama zaidi katika msingi ili nyumba yako iweze kuhimili athari hizo.

EPUKA MAENEO YENYE HATARI ZA KIMAZINGIRA

Hatari za kimazingira huweza kuwa mimonyoko ya ardhi, mionzi hatarishi, maporomoko ya ardhi, mabonde ya mafuriko, maeneo ya vyanzo vya maji, maeneo ya hifadhi za kimazingira. Athari za kimazingira ninamaanisha kwamba wewe unaweza kuathirika vibaya na athari hizo au wewe unaweza kuathiri mazingira vibaya. Ni muhimu kujenga huku ukitunza mazingira kwajili ya kizazi cha sasa na cha baadaye.

Kujenga katika maeneo hatarishi huweza kukuletea hasara za kupoteza mali, magonjwa hata kifo. Mara nyingi serikali imeainisha maeneo hatarishi ya kimazingira japo kuwa taarifa nyingine hazipo wazi. Kama tunavyoona athari ambazo watu wanapata kutokana na mafuriko, maporomoko ya ardhi basi ni vyema kuchagua eneo ambalo lipo katika hali nzuri ya kimazingira.

Katika swala la kutunza mazingira tunazungumzia athali ambayo unaweza kuacha katika mazingira husika. Athari hizo zinaweza kuonekana kwa muda mfupi au mrefu. Maeneo ya vyanzo vya maji na hifadhi za mazingira ni muhimu kuzihifadhi na kuzilinda kwa uhai endelevu wa vizazi vijavyo. Inawezekana pia kuna baadhi ya maeneo bado hayajaainishwa moja kwa moja kwajili ya utunzaji pekee, lakini kuna umuhimu na mujukumu kwa kila mmoja mmoja kuyahifadhi kwa dhati kwani Dunia hii ni sisi ambao tunawajibika katika kuitunza.

BARABARA ZA KUINGILIA

Barabara za kuingilia kwenye kiwanja huunganisha kiwanja hicho na barabara za mtaa mpaka barabara kuu. Hizi barabara ni muhimu kwajili ya kuweka mtiririko mzuri wa shughuli na huduma za kijamii kutoka eneo lako hadi maeneo mengine. Barabara hizi husaidia kuwe na utaratibu mzuri wa shughuli za kila siku bila kubuguzi wengine. Pia husaidia ufanisi wa kudhibiti majanga mbalimbali yanapotokea kama vile moto, wagonjwa n.k. Ununuaji wa kiwanja uhusishe katika kutambua barabara za kuingilia katika kila kiwanja. Viwanja ambavyo havina aina hii ya barabara mara nyingi huleta migogoro ya kijamii.

HUDUMA ZA KIJAMII

Huduma za kijamii husaidia katika kuchangia maendeleo ya kiafya, kiuchumi na kijamii. Huduma hizi hujumuisha huduma za maji safi, huduma za afya, shule, umeme, mawasiliano n.k. Huduma hizi ni muhimu kwajili ya maendeleo ya jamii husika. Huduma hizi huweza kutolewa na serikali au watu binafsi. Umuhimu wa huduma hizi huweza kutofautiana kutoka huduma moja hadi nyingine. Ukaribu na huduma hizi hukusaidia katika kumudu maisha yako kwa urahisi zaidi.

Kuna baadhi ya huduma unaweza kuzipata kwa njia rahisi na bora zaidi kutegemeana na uwezo wa kifedha na kiteknolojia mfano, umeme na maji. Utumiaji wa umeme wa jua, upepo, biogesi husaidia katika kupunguza gharama za uendeshaji na pia husaidia kupunguza kero za kukatika katika umeme. Umeme huu pia husaidia katika kuhifadhi mazingira. Uchimbaji wa visima vya maji, uvunaji wa maji ya mvua husaidia pia katika kupunguza gharama za uendeshaji wa nyumba na kuepuka kero za kukatika katika maji.

Jambo la msingi kabla ya kununua kiwanja chako ni muhimu kuchanganua upatikanaji wa huduma za kijamii utakazo zihitaji. Pia jaribu kutazama njia mbadala za kupata huduma hizo, ubora, gharama n.k kisha hayo yakuongoze katika kufanya maamuzi. Vipi kuhusu huduma za kibenki, usafiri?

Mwisho, ni vyema kupata kiwanja ambacho kitakufaa kwa matumizi ya sasa na ya baadaye kwa watumiaji husika. Swala la gharama za kiwanja ni vyema kulitazama kwa jicho la kiuwekezaji na si kukurupuka tu kisa umepewa ofa ya bei ndogo; nunua ardhi yenye uhakika, itakayokufaa kwa gharama nafuu. Swala la kufuata taratibu za kisheria ni muhimu kwajili ya kupata umiliki halali wa kisheria. Pia ukubwa wa kiwanja utakaokufaa hutokana na matumizi ambayo umekusudia; na upimaji wa kiwanja usifanyike kwa hatua za miguu bali kwa kamba ya kupimia au vifaa vingine vya kitaalamu. Mambo mengine ya kuyazingatia ni barabara za kuingilia, tamaduni, huduma za kijamii, hali ya udongo na ya hewa bila kusahau utunzaji wa mazingira. Usisite kuwatumia wataalamu wa sheria, mabwana ardhi na wataalamu wa majengo ili wakupe ushauri katika uwekezaji wako.

TZ
From TZS 100,000/day
Kinondoni
10 years
Mtaalamu wa mambo ya ujenzi wa makazi aliyesomea na mwenye uzoefu wa muda mrefu, kutoka kwenye kusanifu ramani za nyumba, usanifu wa nadharia ya nje ya nyumba na bustani, pamoja na mambo ya makisio na mahesabu ya gharama za ujenzi. Lengo letu ni kukuwezesha kutimiza nyumba ya ndoto yako sasa, bila kujalisha kama ni ya gharama nafuu au mjengo wa heshima.
3D Rendering Building Designing Cost Estimation Landscape Designing Project Management Project Planning Technical Drafting

WhatsApp Image 2019-09-16 at 09.38.52

ID-16960
3
210 sqm
86 Pcs
16 m
5,040 Pcs
15 m
1,869 Pcs

POST 12-1a

ID-17859
3
131 sqm
90 Pcs
15 m
2,345 Pcs
11 m
1,166 Pcs

POST 44 – 3

ID-17034
5
222 sqm
135 Pcs
15 m
4,168 Pcs
13 m
1,775 Pcs

MSH_Photo – 62B_Photo – 71

ID-7823
3
84 sqm
65 Pcs
12 m
1,200 Pcs
9 m
645 Pcs

452784405114628560378503383796837654202546n

ID-15178
3
162 sqm
84 Pcs
15 m
3,279 Pcs
13 m
1,442 Pcs

467362932830533823507548836387209714501851n

ID-15169
3
149 sqm
77 Pcs
14 m
2,667 Pcs
14 m
1,326 Pcs

MGF 1_Photo – 21

ID-26412
4
524 sqm
108 Pcs
19 m
16,277 Pcs
18 m
3,732 Pcs

POST 17-3

ID-17823
4
189 sqm
130 Pcs
16 m
3,383 Pcs
15 m
1,682 Pcs

54247846_129004444892786_1287105494891443325_n

ID-15144
4
214 sqm
131 Pcs
15 m
4,340 Pcs
14 m
1,100 Pcs

ABBY 5_Photo – 23a

ID-21918
5
555 sqm
0 Pcs
19 m
18,101 Pcs
14 m
2,823 Pcs

SAGAYA_Photo – 9A

ID-13362
4
243 sqm
136 Pcs
21 m
4,072 Pcs
15 m
2,059 Pcs

PLN 12_Photo – 24

ID-19472
1
103 sqm
42 Pcs
12 m
2,472 Pcs
12 m
917 Pcs