FANYA HIVI KUPUNGUZA GHARAMA ZA UJENZI

TZ
From TZS 100,000/day
Kinondoni
10 years
Mtaalamu wa mambo ya ujenzi wa makazi aliyesomea na mwenye uzoefu wa muda mrefu, kutoka kwenye kusanifu ramani za nyumba, usanifu wa nadharia ya nje ya nyumba na bustani, pamoja na mambo ya makisio na mahesabu ya gharama za ujenzi. Lengo letu ni kukuwezesha kutimiza nyumba ya ndoto yako sasa, bila kujalisha kama ni ya gharama nafuu au mjengo wa heshima.
3D Rendering Building Designing Cost Estimation Landscape Designing Project Management Project Planning Technical Drafting

 

Moja ya mambo ambayo yamekuwa yakishughulisha na kufikilisha akili za watu wengi ni swala la ujenzi. Jambo ambalo haswa limekuwa lenye kusababisha hiyo tafakari kubwa ni namna ya kuweza kufanikisha gharama zinazohitajika. Gharama ni jumla ya nguvu, rasilimali na uwezo ambao unahitajika ili uweze kupata kitu ambacho unakitaka.

Katika ujenzi, gharama huangukia katika rasilimali watu na vitu; hizo ni gharama za ufundi pamoja na nyenzo za ujenzi. Katika ulimwengu wa sasa ambapo teknolojia imeendelea zaidi, ujenzi wa nyumba umekuwa ni kitu ambacho kinahitaji utaalamu mkubwa ili uweze kukidhi sheria na tamaduni zilizopo. Miaka ya zamani ilikuwa inawezekana kujenga nyumba kwa namna ambayo unataka mwenyewe ambapo ingeweza kuwa na gharama ndogo zaidi; lakini miaka ya sasa tamaduni na sheria zimekuwa zikilazimu kwa namna moja au nyingine kujenga nyumba yenye kiwango fulani cha ubora.

Ni muhimu kujenga nyumba ambayo imekidhi viwango vya kitaalamu na kisheria kwa manufaa yetu wenyewe. Watu wengi wamekuwa wakilalamika ughali wa gharama unaotokana na kujenga kwa kufuata taratibu za kitaalamu; basi ni muhimu kujua kwanini gharama hizo zinazaliwa.

Zipo sababu nyingi za msingi ambazo zinafanya swala la ujenzi liwe la gharama kubwa; moja ya sababu ni uwekezaji. Uwekezaji unatabia ya kuiweka mali katika mfumo fulani ili baada ya muda fulani uje upate faida fulani. Mfumo huo unaweza kuwa na taratibu zinazopaswa kufuatwa ili uweze kupata jibu lenye matokeo mazuri ya faida. Katika ujenzi kama uwekezaji, ni lazima ufuate vigezo vya usalama, ubora, afya, kudumu, uimara na vingine vingi ili mfumo huo wa uwekezaji katika ujenzi ufanye kazi vizuri na kuleta matokeo mazuri. Hii ikimaanisha, gharama za ujenzi huzaliwa pale tunapofuata kutimiza vigezo vya kiuwekezaji katika ujenzi; kwa hiyo kulipia gharama katika ujenzi ni muhimu ili uwekezaji wako upate kuwa wenye tija. Wataalamu na watu wa fani husika wamefanikiwa kuvijua na kuviweka wazi vigezo ambavyo unapaswa kuvifuata ili upate kujenga nyumba ambayo ipo katika ubora na faida ya kiuwekeaji. Vigezo hivyo huangukia katika ufundi na nyenzo unazopaswa kuzitumia ili kukamilisha ujenzi wako kwa ufanisi.

Licha ya kuwepo na vigezo na gharama, bado kitaalamu kuna nafasi ya kuweza kupunguza gharama zisizo na lazima bila kuharibu ubora wa nyumba. Mwanafalsafa mmoja alisema ili uweze kufanikiwa zaidi katika kazi yako kuliko wengine, unapaswa uwe na mfumo ambao una ufanisi wa kazi zaidi kuliko wengine. Ufanisi tunaozungumzia hapa ni kuweza kuzalisha kitu kilicho bora zaidi kwa gharama ndogo zaidi.

Mambo ambayo tunaweza kuyafuata ili tuweze kupunguza gharama za ujenzi bila kuharibu ubora wa kazi, yameangukia katika mifumo mitatu. Mifumo hiyo ni

  • Usanifu
  • Manunuzi
  • Ujenzi

1.    USANIFU NA MIPANGO

Usanifu ni kufanya maamuzi na kuamua namna ambapo jengo na mifumo yake yote inavyopaswa kuwa ili ifanye kazi katika ufanisi unaohitajika. Hii hujumuisha mwonekano, miundo, umeme, maji, mandhari na kila kitu kinacho husiana na nyumba.

Hii ni hatua ya kwanza naya msingi katika ujenzi. Unapokosea katika hatua hii basi hata mwisho kuna uwezekano mkubwa sana wa kukosea. Ni muhimu kufanya maamuzi ya msingi katika hatua hii. Ni muhimu kupata wataalamu ambao wamebobea katika kufanya kazi hii ya usanifu ili uweze kuweka msingi mzuri wa nyumba yako. Hatua hii huweza kuhusika pia katika kukadilia gharama ambazo nyumba yako itagharimu na muda ambao utahitajika kukamilisha ujenzi wako.

Mambo unayoweza kuyachukua katika hatua hii ili kupunguza gharama za ujenzi ni

a.                  Jenga nyumba ile ambayo unaihitaji

Hii inamaanisha kuwa kuna watu wanajenga nyumba ambazo hawazihitaji au hazitawasidia kwa muda ambao wamekusudia. Kujenga nyumba ambayo ni kubwa sana au ndogo sana ni sawa na kujenga nyumba ambayo huihitaji. Hakikisha umekaa makini na mtaalamu wako na kujadiliana katika mahitaji uliyonayo na dukuduku nyingine unazozipenda ili uwe umelidhika na nyumba ambayo utaijenga.

b.                 Tumia nafasi za eneo vizuri

Hii ni moja ya njia ya kitaalamu katika kupunguza gharama. Kila ongezeko la eneo la mita moja ya mraba katika nyumba yako inagharimu wastani wa Tsh. 500,000/=, kwa nyumba ya kawaida. Hii inakupa picha kwamba hupaswi kuwa na nyumba ambayo inachukua eneo kubwa bila ya sababu ya msingi. Hii inakwenda sambamba na kutumia nafasi wima (mfano: kutumia makabati ya ukutani) ambayo mara nyingi imekuwa kama haitumiki. Punguza mita za mraba za nyumba zisizo za lazima.

Hii inakwenda pamoja na kuepuka kuwa na korido zisizo na ulazima. Korido zinaweza kuongeza ukubwa wa nyumba mpaka 30%.

Epuka kuwa na nyumba yenye konakona na umbo gumu; nyumba yako iwe na mwonekano rahisi lakini mzuri.

a.                  Epuka kuweka vitu na urembo usio wa lazima.

Kuna baadhi ya vitu ambavyo tunaviweka katika nyumba zetu pindi tunapojenga havina ulazima bali vinaongeza urembo tu. Unaweza tumia kibaraza cha bati badala ya nzege. Unaweza kuachana na madirisha ya aluminiamu na kutumia madirisha ya nyavu tu. Unaweza kuacha kujengelezea makabati vyumbani kwani yanaweza kuongeza gharama za maofali na saruji.

b.                  Jaribu kutumia teknolojia mbadala

Teknoloia za ujenzi zipo nyingi na zenye ubora na gharama tofauti tofauti. Ni muhimu kuweza kuziangalia hizo teknolojia kama zitaweza kufaa mradi wako huku ukiangalia swala la gharama. Kuna teknoilojia za nyumba za makontena, paneli, matofali ya kushikana, nyumba za mbao n.k. Pia unaweza kuangalia swala la umeme wa bayogesi, nguvu ya jua n.k; jaribu kuangalia swala la kuezeka kwa kutumia mianzi na teknolojia nyingine. Ukifungua macho katika teknolojia nyingine unaweza kupata teknolojia inayokufaa wewe na ambayo ni ya gharama nafuu.

c.                   Pangilia mradi wako kitaalamu

Katika hatua hii ya kusanifu na kupangilia, ni muhimu kupangilia kazi yako vyema kwa jinsi itakavyofaa mradi wako. Sanifu kitu ambacho kipo halisi na kinajengeka. Kuweka mradi wako katika maandishi na katika mifumo ya kitaalamu kutasaidia kufuatilia utekelezaji pindi mtakapokuwa mnajenga. Kazi ambayo imehifadhiwa vizuri huweza kufanywa na mtu yeyote yule ambaye unaujuzi husika. Pangilia mradi wako vizuri huku ukijua gharama zinazohitajika, wapi utakapokwenda kununua vitu vyako, rasilimali watu ipi inayohitajika, muda unaohitajika kukamilisha mradi wako n.k.

2.    MANUNUZI

a.             Nunua vifaa vilivyo bora, halisi na utumie wataalamu walio na uwezo, ustadi, uhodari na ufarisi unaotakiwa!

Moja kati ya mambo ambayo yanahitaji hekima na busara katika ujenzi ni ununuaji wa vifaa vinavyotakiwa. Mara nyingi vifaa halisi na vyenye ubora vimekuwa vina gharama kubwa kuliko vifaa bandia; wengi wamekuwa wakifanya maamuzi yasiyo sahihi kwa kununua kwa kuangalia bei tu bila kuangalia ubora unaotakiwa. Faida ambayo unaweza kuipata kwa kununua vifaa halisi na vyenye ubora ni

  • Kupata kifaa kilichokubalika kitaalamu kwa matumizi husika
  • Kupata kifaa kitakacho dumu kwa muda mrefu zaidi huku kikiokoa gharama za muda mrefu
  • Kupata kifaa kinachokidhi afya ya watumiaji na kutunza mazingira
  • Kuchangia kukuza pato la taifa kiuchumi

Hasara za kutumia vifaa vya ujenzi ambavyo ni duni na bandia ni nyingi ikiwa ni pamoja na kujenga nyumba duni, kuingia gharama za ukarabati kila baada ya muda mfupi, ubomokaji wa jengo na vifo kwa watumiaji wa jengo.

Hii huenda sambamba pamoja na kutumia wataalamu walio na uwezo, ustadi, uhodari na ufarisi unaotakiwa. Teknolojia imekua, biashara imekua; nyumba zinazojengwa miaka ya siku hizi ni kubwa, pana, nzito kwa nyepesi, zinazotumia vifaa vya kisasa na zinahitaji ujuzi wa sayansi na sanaa kwa undani zaidi. Hakikisha unajua ni kiwango gani cha utaalamu unaohitajika ili kuweza kufanikisha mradi wako. Ni bora zaidi kupata mtaalamu aliyebobea na mwenye uzoefu zaidi ili kufanya kazi yako kwa uhakika zaidi.

Taratibu na sheria zinaelekeza pia kutumia makampuni kwa aina fulani ya miradi kama ujenzi wa maghorofa; hakikisha unafuata taratibu na kupata kampuni inayofaa kwajili ya kazi yako. Ijapokuwa kuna gharama katika kutumia wataalamu na makampuni yenye ubora unaotakiwa, ni muhimu kufanya hivyo kwajili ya uhakika na ubora wa mradi wako. Hakikisha unapata wataalamu waliojitoa kwa dhati kushirikiana nawe katika kufanikisha mradi wako. Jifunze kulipia gharama inayotakiwa ili upande kiwango cha juu zaidi.

b.            Tambua gharama katika soko

Ni muhimu kujua gharama ya manunuzi sokoni ipoje; hii ni gharama ya vifaa na wataalamu. Tembelea tovuti, madukani, kwa wenzako ambao wameshafanya ujenzi ili ujue gharama ipoje. Hii itakusaidia kujua kiasi cha fedha kinachohitajika ili ujipange vyema.

Hii inakwenda sambamba na kutafuta soko lenye gharama nafuu zaidi. Unaweza kupata mtu anayeuza vifaa unavyovihitaji kwa gharama nafuu zaidi. Unaweza kupata mbao za zege zinazouzwa kwa gharama nafuu zaidi.

c.      Nunua na safirisha kwa ujumla

Moja ya mambo ambayo yanaweza kukusaidia kupunguza gharama ni pale utakapo nunua vifaa kwa ujumla. Unaweza nunua saruji kwa jumla kiwandani na ukaokoa gharama kubwa. Unaweza nunua mbao msituni kwa jumla na ukaokoa gharama. Unaponunua vifaa vingi kwenye duka moja waweza pewa punguzo la bei.

Hii ni sambamba na usafirishaji; waweza kununua tofali na saruji kwa pamoja huku ukavisafirisha vyote kwa pamoja na kuokoa nauli. Unaponunua vifaa kwa pamoja na kuvisafirisha vyote kwa pamoja inasaidia kuokoa gharama ya nauli.

d.     Patana na fundi kufanya kazi kwa pamoja

Hii inamaanisha kuwa waweza mpa fundi kazi ya kujenga msingi, kuta na kupiga lipu nyumba nzima kwa pamoja huku bei ya ufundi mkapatana kwa ujumla wa kazi yote; gharama utakayomlipa itakuwa nafuu zaidi kuliko kama mkapatana kwa kazi moja moja. Gharama utakayomlipa fundi kupaua nyumba na kupiga dari kwa pamoja itakuwa nafuu zaidi kuliko akipaua fundi huyu na kupiga dari fundi mwingine. Jambo la msingi hapa ni kupata fundi ambaye anaweza kufanya kazi za aina mbalimbali na kwa ubora zaidi.

e.      Nunua baadhi ya vifaa kabla

Hii pia ni njia nzuri ya kuokoa gharama zako za ujenzi. Waweza anza kununua baadhi ya vifaa mapema na polepole; waweza nunua tofali, mawe, mchanga na ukavihifadhi vizuri pindi unapokuwa umepata kiasi fulani cha pesa kidogo kidogo. Waweza tengeneza madirisha na milango mapema pale unapokuwa umepata kiasi fulani cha pesa. Njia hii inaleta maana zaidi pale unaponunua vifaa pindi vinapokuwa na bei nafuu zaidi au mtu anapokuwa anaviuza kwa gharama nafuu. Umuhimu wa kupangilia mradi wako na kujua makadilio ya gharama yake unaonekana pia hapa kwasababu utanunua vifaa vile vinavyohitajika tu.

f.       Fanya makubaliano ya bei, omba punguzo la bei na tunza risiti na mikataba

Ni muhimu kujua undani na mchanganuo wa gharama wa vifaa na ufundi ili uweze kufanya maamuzi yenye busara kuhusiana na bei. Kutokujua undani wa mradi wako inaweza kusababisha kulipia gharama zaidi.

Wakati mwingine ni muhimu kufanya makubaliano ya bei kwani bei yeyote ile ya kitu au huduma hupangwa na watu kulingana na wao wanavyoona; hii inaweza kukusaidia kupata nafasi nzuri ya kulipia kwa unafuu zaidi. Kuna baadi ya wauzaji wamekuwa wakiweka bei juu zaidi ili mtakapo kubaliana muweze kushuka mpaka bei anayoitaka yeye. Negotiation ifanyike kwa busara na ukweli huku pande zote mbili zikiridhika na muafaka wa makubaliano. Ni muhimu kujua kufanya makubaliano yaliyo mazuri.

Omba punguzo la bei ili nawe uweze kuongeza zaidi thamani ya fedha yako. Pia pale unapokuwa umepungukiwa kiasi fulani cha fedha waweza omba punguzo ili uweze kufanikisha manunuzi yako. Pia Unaponunua vifaa vingi kwa pamoja waweza omba ofa ya punguzo la bei.

Kumbuka kutunza mikataba na risiti za manunuzi kwajili ya matumizi ya baadaye. Hii inakwenda sambamba na kurekodi manunuzi katika daftari lako maalumu ili uweze kutumia taarifa hizo kufanya maamuzi yaliyo sahihi siku za mbeleni.

3.    UJENZI

a.        Usikisie, jenga kulingana mipango ya kitaalamu iliyowekwa

Hapa ninazungumzia kuhusu kujenga nyumba yako kulingana na ramani na mipango ya kitaalamu ambayo imeshafanywa. Mipango hii ya kitaalamu inajumuisha ramani, makadilio ya gharama za ujenzi, mipango ya uratibu mradi iliyowekwa.  Hii inasaidia kutekeleza mradi wako kwa uhakika.

Hasara za kujenga bila kufuata mipango ya kitaalamu iliyowekwa ni

  • Ongezeko la gharama kubwa zaidi
  • Kujenga bila kujua mnakokwenda
  • Mradi wako kukumbwa na mabishano, ushindani, ubishi, mzozano, migogoro, kutokubaliana
  • Kujenga kilicho kibovu na kisicho na ubora
  • Kujenga bila kufuata taratibu na sheria husika

Ni muhimu kujenga kwa kufuata taratibu za kitaalamu na sheria husika. Mipango ya kitaalamu inasaidia kujua mnakokwenda na ni msingi wa maboresho ya mradi wako. Mara nyingi mabadiliko katika mradi yamekuwa yakipelekea kuongezeka kwa gharama za ujenzi.

b.     Fuatilia kwa ukaribu na undani zaidi jinsi mradi wako unavyokwenda

Ni muhimu kujua namna kazi na mambo yanavyokwenda katika mradi wako. Hakikisha unayajua vizuri zaidi hata kabla hamjaanza. Jua kwa undani zaidi kwanini hiki kipo hivi na kile kipo vile; kwanini wanaweka nondo nne badala ya tatu; kwanini utachukua miezi miwili kukamilika?

Siku zote unapojiuliza swali ‘kwanini’, basi waweza jua undani na sababu hivyo waweza kuboresha zaidi.

Hata kama upo mbali na umetingwa na majukumu, basi waweza pata mwangalizi ambaye yupo makini zaidi; ijapokuwa umakini na ukaribu wako bado ni muhimu zaidi.

c.      Kagua mahesabu yako

Siku zote kile kilicho pangiliwa huwa hakiendi sawasawa kwa asilimia zote, bali huwa kuna marekebisho na mabadiliko kiasi. Ni muhimu kukagua mahesabu ya mradi wako ili kujua wapi yamepanda, yameshuka au yapo sawasawa ili uweze kufanya maamuzi yaliyo sahihi. Hii inakwenda sambamba na kulinganisha kilicho pangwa na kilicho fanywa katika gharama, muda na kazi. Tambua sababu za utofauti na usawa; toa maamuzi yaliyosahihi ili kuboresha mradi wako. Mfano, unaweza kuta sokoni kuna ongezeko kubwa la bei ya madirisha na milango ya mbao kulingana na makadirio yenu mliyoweka, basi mtu mwingine anaweza fanya  maamuzi ya kubadili aina ya madirisha na milango na kutumia ya aina nyingine yenye gharama nafuu zaidi.

d.     Zuia na epusha wizi, ufujaji, uvujaji na uharibifu

Moja ya vitu vinavyoweza kutokea na kuongeza gharama za ujenzi bila kutarajia katika mradi wako ni wizi, ufujaji, uvujaji na uharibifu. Haya mambo yanahitaji ujuzi na umakini wa kuyaepuka. Waweza nunua mbao kwa gharama kubwa kisha zikaoza na kuwa hasara; swala la kuoza linaweza kuepukika.

Inahitaji umakini kuepuka wizi, ufujaji, uvujaji na uharibifu katika mradi wako. Umakini unahitajika katika kuandaa mradi na kuutekeleza. Baadhi ya mambo yanayoweza kukusaidia kuepuka hayo mambo ni

  • Fanya makadilio mazuri ya gharama, nunua vinavyohitajika tu na fanya ukaguzi mzuri wa mahesabu ya mradi wako – hii itakusaidia kujua ni kipi kinachohitajika na kwa gharama gani; ni wapi mahesabu yalipochepuka na kwanini. Kipengere hiki kitakusaidia kuona ni wapi ulipoibiwa na ni lini. Tumieni vifaa kwa umakini bila ufujaji; pangilia vizuri kazi yako kabla ya utekelezaji kuendelea.
  • Tumia watu waaminifu na wenye uhodari katika mradi wako – watu unaoshirikiana nao katika kufanya kazi hasa mafundi na wasimamizi wanaweza kuleta hasara kwa kuiba au uzembe. Kitu cha kwanza ni kufanya kazi na mtu mwaminifu ambaye unaweza mpata kwa kuangalia tabia na historia yake.
  • Fuatilia kwa ujirani na undani zaidi namna mradi wako unavyokwenda – hii ninazidi kusisitiza ili kujua hali zinavyokwenda katika mradi wako na kuzipa maamuzi sahihi. Kutokuwa jirani na mradi wako kunaweza kusababisha kupokea taarifa zisizo na ukweli kuhusu kazi yako na kuingia hasara. Unapokuwa jirani na mradi wako utajua kuwa ni kweli nondo kadhaa zimewekwa, saruji kiasi kadhaa imetumika sawasawa, zege linalokubalika kitaalamu limewekwa. Ujirani wako unasaidia kupunguza mianya ya wizi na udanganyifu.
  • Tambua na tumia njia nzuri kutunza vifaa vya ujenzi – hapa ujuzi unahitajika kujua namna ya kuhifadhi vifaa vyako. Mbao hazihitaji unyevunyevu, jua kali sana na zisipinde; pia kuna baadhi zinapaswa zipigwe dawa ya wadudu. Saruji haihitaji unyevunyevu pia usikae nayo sana stoo. Tumia wataalamu kukushauri namna ya kutunza vifaa vyako.
  • Weka ulinzi na usalama wa kutosha katika mradi wako – kiasi cha ulinzi kinachohitajika kinategemea mradi na mradi kulingana na mazingira yake. Wizi unaweza kutokea kutokana na watu wa ndani ya mradi au nje ya mradi. Pia inatakiwa kuhakikisha usalama unakuwepo wa kutosha ili watu na vyote katika mradi visidhurike. Inatakiwa kuhakikisha usalama wa kutosha kwa walio nje na ndani ya mradi.

Mwisho, upunguzaji wa gharama za ujenzi katika mradi wako hauhusishi kutumia vifaa vilivyo duni na wataalamu wasio hodari na ujuzi, bali ni umakini na utaalamu wa kuweza kuendesha mradi wako kwa ufanisi zaidi na gharama nafuu bila kuharibu ubora na afya ya mradi. Hii inajumuisha kutambua mianya ambayo inapaswa kuzibwa ili kupunguza gharama zisizohitajika na kutambua fursa zinazohusiana na mradi wako ili uweze kuongeza ufanisi wa kazi yako. Hakikisha unajenga unachohitaji, kilicho bora, kinachodumu na imara. Usisite wala kuogopa kutumia wataalamu kufanikisha mradi wako kwa ufanisi na uhakika zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TZ
From TZS 100,000/day
Kinondoni
10 years
Mtaalamu wa mambo ya ujenzi wa makazi aliyesomea na mwenye uzoefu wa muda mrefu, kutoka kwenye kusanifu ramani za nyumba, usanifu wa nadharia ya nje ya nyumba na bustani, pamoja na mambo ya makisio na mahesabu ya gharama za ujenzi. Lengo letu ni kukuwezesha kutimiza nyumba ya ndoto yako sasa, bila kujalisha kama ni ya gharama nafuu au mjengo wa heshima.
3D Rendering Building Designing Cost Estimation Landscape Designing Project Management Project Planning Technical Drafting

OK_Photo – 27

ID-13597
2
185 sqm
129 Pcs
23 m
4,382 Pcs
10 m
1,391 Pcs

ID-18101
3
177 sqm
73 Pcs
17 m
4,236 Pcs
14 m
1,571 Pcs

DUHU_Photo – 51A

ID-28592
10
1,041 sqm
0 Pcs
22 m
27,622 Pcs
20 m
6,500 Pcs

MARTHA_Photo – 54

ID-10075
3
175 sqm
120 Pcs
12 m
3,366 Pcs
11 m
811 Pcs

15

ID-14974
4
266 sqm
115 Pcs
22 m
5,000 Pcs
16 m
2,500 Pcs

POST 57-3

ID-16988
3
144 sqm
99 Pcs
13 m
2,578 Pcs
12 m
1,282 Pcs

IMG-20220216-WA0006-01

ID-8010
4
138 sqm
108 Pcs
15 m
2,160 Pcs
13 m
1,164 Pcs

POST 73 – 2

ID-17622
3
404 sqm
175 Pcs
22 m
10,725 Pcs
13 m
3,095 Pcs

FRANCISCA_Photo – 11

ID-14023
4
141 sqm
112 Pcs
15 m
2,112 Pcs
12 m
1,211 Pcs

MOYO_Photo – 19~2

ID-28439
2
64 sqm
59 Pcs
12 m
1,150 Pcs
5 m
572 Pcs

43103339_292392231606509_8219117807478237936_n11

ID-15474
4
192 sqm
153 Pcs
17 m
3,437 Pcs
14 m
1,704 Pcs

ID-33409
7
516 sqm
149 Pcs
15 m
13,716 Pcs
18 m
3,206 Pcs

Join Membership

Join our membership to become a part of our expansive platform dedicated to residential development in Africa. Gain access to house plans, informative articles, vetted builders, plot listings and construction materials!

Eng. Lwifunyo Mangula
Payment Challenges? WhatsApp Admin