UDHIBITI WA TAKA KATIKA NYUMBA NA MIFUMO YAKE

TZ
From TZS 100,000/day
Kinondoni
10 years
Mtaalamu wa mambo ya ujenzi wa makazi aliyesomea na mwenye uzoefu wa muda mrefu, kutoka kwenye kusanifu ramani za nyumba, usanifu wa nadharia ya nje ya nyumba na bustani, pamoja na mambo ya makisio na mahesabu ya gharama za ujenzi. Lengo letu ni kukuwezesha kutimiza nyumba ya ndoto yako sasa, bila kujalisha kama ni ya gharama nafuu au mjengo wa heshima.
3D Rendering Building Designing Cost Estimation Landscape Designing Project Management Project Planning Technical Drafting

Tuzungumze kuhusu swala zima la kudhibiti taka katika nyumba zetu za kuishi bila kujali ni ya kwako au ni ya kupanga. Kwanza, maana ya takataka ni kitu au vitu ambavyo havifai tena, havitumiki tena, si vya muhimu tena. Japo hiyo tafsiri haijakamilika vizuri.

Tafsiri nyingine inasema kwamba, takataka ni vitu ambavyo kwa muda huo si vya muhimu tena baada ya mtumiaji wa muda huo kutokuwa na matumizi navyo tena, hivyo hutaka kuvitupa au tayari ameshavitupa! Ni vitu ambavyo aliyenavyo yupo katika maamuzi ya kuvitupa au hutaka kuvitupa. Vitu hivi huwa vimetoka kutumika katika uzalishaji, ubadilishaji au ulaji.

Aina ya taka huweza kugawanywa kutokana na namna mbalimbali za uchambuzi. Huweza kugawanywa katika hali zake za kiumbo kama vile taka-maji na taka-ngumu. Pia huweza kugawanywa kutokana na mifumo ya uzalishaji na athari zake; mfano taka za hospitali, majumbani, za kikemikali, viwandani n.k.

Maana ya kudhibiti taka ni hatua na michakato yote inayopaswa kufanywa tangu hatua ya awali kabisa ya kutengeneza taka hadi hatua ya mwisho ya kutupa taka ambayo ina lengo la kupunguza athali za taka kwa afya na mazingira. Mifumo hii hujumuisha tangu ukusanyaji, usafirishaji, kuzitibu na kuzitupa. Mifumo hii ni ya kitaalamu japo mingine tunaifahamu na tunaitumia katika maeneo yetu. Lengo la kudhibiti taka ni kupunguza athari mbaya za taka kwa afya na mazingira.

Leo tutazungumzia hatua za msingi katika kukabiliana na takataka katika makazi yetu. Hatua hizi ni za msingi katika maeneo yote yale ambayo huhusika na kudhibiti taka, japo sisi tutazitazama katika mazingira ya nyumbani.

JIZUIE NA PUNGUZA KETENGENEZA TAKA

Hapa tunazungumzia kupunguza kiasi cha ujazo wa takataka zinazotengenezwa bila kuongeza athali ya taka zinazotengenezwa. Hii inasaidai kupunguza kiasi cha athali kwa afya na mazingira. Kitaalamu shughuli yeyote ya awali kabla ya kutengeneza taka, ambayo itakusaidia kupunguza ujazo wa takataka bila kuongeza athali ya taka inahusika katika kipengere hiki. Baadhi ya hatua unazoweza kuchukua nyumbani ni

  • Nunua vitu vile tuu ambavyo unavyovihitaji. Pia unashauriwa kuwa na tabia ya kununua vitu kwa jumla ili kupunguza kiasi cha vifungashio ambavyo baadaye hujakuwa taka. Tumia vikapu maalumu vya kudumu kwajili ya kubebea mizigo badala ya kutumia mifuko ya plastiki ya madukani.
  • Jifunze kununua vitu vile ambavyo vinadumu kwa muda mrefu ili usinunue mara kwa mara. Uza au wape watu wengine vile vitu ambavyo huvihitaji kama vyakula, nguo, makopo na vinginevyo.
  • Punguza utumiaji wa karatasi kwa kutumia kompyuta na vifaa vingine mbadala
  • Tumia vitu mpaka vinaisha ili kupunguza takataka
  • Hifadhi vitu vile ambavyo vinaweza kutumika baadae ili visiwe taka. Hii hujumuisha vyakula, kemikali, fanicha, karatasi na vinginevyo.
  • Azima au kodi baadhi ya vitu badala ya kuvinunua. Kuna vitu kama vile mbao za kupigia nzege ambazo unaweza kukodi. Kwa mambo ya kupulizia dawa za wadudu, unaweza kukodi kampuni badala ya kupuliza kwa kutumia vifaa vyako mwenyewe ambavyo itakubidi kuvinunua.

Kwa kufuata hatua hizi unaweza kupunguza asilimia kubwa ya taka unazotengeneza pale nyumbani kwako. Kipengere hiki unaweza kukijumuisha tangu katika ujenzi wa nyumba yako; Mfano, nunua kiasi kinachohitajika tu cha vifaa vya ujenzi kama vile rangi, mbao, saruji n.k. Pia ununuaji wa vifaa vile ambavyo ni bora na ambavyo vinadumu kwa muda mrefu. Badala ya kununua rangi kwenye makopo ya lita 4, basi nunua katika ndoo za lita 20.

ZIPE TAKA MATUMIZI MBADALA

Awali katika tafsiri ya taka nilielezea kwamba takataka sio taka, bali ni taka kwasababu huyo mtu hazihitaji, kwa hiyo bado zina thamani kwa mwingine. Kipengere hiki kinahamasisha kutambua thamani ya taka ulizonazo na kuzipa matumizi mbadala ambayo yataleta faida.

Tukianza na maji-taka; jaribu kuyapa maji-taka matumizi mbadala. Hii inaanza tangu bafuni kwenda jikoni hadi nje uani.

  • kwa chooni unaweza kutumia sinki za kunawia mikono ambazo maji yake yaliyotumika hutumika tena kuflashi choo. Hii husaidia kupunguza kiasi cha uzalishaji wa maji-taka na gharama za maisha.

Maji yaliyotumika kuoshea matunda na mbogamboga yanaweza kutumika kumwagilia bustani. Maji yaliyotumika kufulia huweza kutumika kudeki na kusafisha choo.

  • Vuna maji ya mvua ili yatumike katika matumizi mbalimbali. Uvunaji wa maji ya mvua huweza kukusaidia upunguze kero za maji. Maji haya yanaweza kukusaidia kwa kipindi kirefu katika mwaka. Kuna matumizi ambayo hayahitaji maji yaliyotibiwa kama vile kumwagilia maua na ukoka. Pia inaweza hitajika maji yatibiwe ili yatumike kwa matumizi mengine kama usafi, kupika n.k. Vitu vya msingi katika kuvuna maji ya mvua ni kuhakikisha kwamba kifaa kinachotumika kuvuna maji ya mvua hakitoi sumu; hii ikimaanisha kwamba kuna baadhi ya vifaa kama baadhi ya bati za nyumba huwa na sumu kama vile kutu n.k. Hakikisha maji yako yanatibiwa kuondoa takataka na harufu. Na pia unapo hifadhi maji hakikisha hayapigwi na mwanga kwani mwanga huchangia uzalianaji wa vijidudu kama vile lava; hivyo kuwe na mfumo ambao utakusaidia kuhifadhi maji bila kuleta mwanga. Mara nyingi tunaweka tanki kubwa ambalo hujengwa na kufukiwa ardhini kwa kuhifadhi maji kwa muda mrefu na pia kuna kuwa na tanki dogo juu kwajili ya maji ya matumizi ya muda mfupi.

Uvunaji wa maji ya mvua hujumuisha pia yale maji ambayo humwagika katika sehemu za wazi kama vile paving blocks na nyua; maji haya yanapokusanywa huweza kutumika kwa umwagiliaji n.k. Ni muhimu kuwasiliana na wataalamu kukutengenezea mfumo ambao umekaa makini utakaodumu.

 

  • Mkojo sio takataka; mkojo ni mali kubwa sana. Kitaalamu mkojo una kemikali muhimu ambazo zina virutubisho vya mimea. Kiasi cha virutubisho vilivyo katika mkojo ni vingi sana kiasi cha kuweza kuunguza mmea kama uki utumia vibaya. Virutubisho hivyo ni Urea. Kuna baadhi ya nchi zinakusanya mkojo kati maeneo ya umma na kuutumia katika kilimo cha mbogamboga; matokea yake yapo chanya. Jambo la msingi katika mikojo ni kuhakikisha kwamba usiwe na vijidudu vya magonjwa na pia upate kuwekwa katika mmea kwa namna inayofaa. Kiukweli tumejaliwa rasilimali nyingi sana, akili tu inapaswa kutumika. Hii pia inaweza kufanywa kuwa biashara yenye tija nzuri kabisa. Tunataka tuone Watanzania ambao wanakuwa wabunifu na kuleta faida katika jamii. Changamkia fursa!
  • Sambamba na mkojo kama mbolea, pia kinyesi kinaweza kutumika kama mbolea. Kwa kweli hizi ni teknolojia zilizokuwa tangu miaka ya zamani, kinachotakiwa ni utayari wa kuzitumia katika jamii. Kinyesi kinapaswa kudhibitiwa vizuri ili kiweze kutumika kwa matumizi mengine. Pia ni muhimu kubadili mtazamo wa watu kuhusiana na matumizi ya mkojo na kinyesi. Ni jambo la kushangaza kama tutazidi kulalamika maisha magumu wakati bado tumezungukwa na fursa mbalimbali.
  • Tengeneza mfumo mzuri wa kudhibiti maji yenye usabuni ambayo yanaweza kutoka maeneo ya bafuni, jikoni na kufulia. Kwa kutumia teknolojia ya kuchuja mafuta na kusafisha maji kwa kutumia mchanga na mimea jamii ya tete pamoja na teknolojia ya kuua viini vya maradhi, waweza kuyatumia tena maji ambayo yana usabuni. Tizama mfumo katika picha hiyo chini. Mfumo huo utakapotumika waweza kukusaidia kupunguza kiasi cha maji taka pamoja na upunguzaji wa gharama ya kodi ya maji. Hivi ni vitu ambavyo vinaweza kabisa kutumika katika nyumba zetu ili mradi nia na ufahamu uwepo. Kitu cha msingi ni kuyatibu maji hayo vizuri pamoja na kuhakikisha kwamba mifumo inafanya kazi bila kukwama kwa kuziba.

Taka ngumu zaweza kutumika kwa matumizi mbadala mengi, jambo la msingi ni kuhakikisha kwamba zinatumika bila kuwa na sumu.

  • Vyakula vilivyobaki vinaweza kutumika kulishia mifugo kama vile paka, mbwa n.k
  • Nguo ambazo hazitumiki zaweza kupewa matumizi mengine kama kudekia, kutengenezea makochi au sehemu yeyote inayofaa kuzitumia
  • Mabaki ya vitu vinavyooza vyaweza kutumika kutengenezea mbolea kwajili ya kilimo, cha msingi ni kuhakikisha kwamba hazina sumu na hatari za kiafya
  • Waweza kubadili ndoo za rangi kuwa makopo ya maua
  • Waweza kutumia nzege iliyobomolewa kuwa mawe kwajili ya ujenzi
  • Kuna baadhi ya maeneo wametumia makopo ya maji ya kunywa kuwa mapambo ya pazia; wapo wengine ambao wametumia kwajili ya ujenzi wa nyumba.

Kwa ujumla, twaweza kubadili takataka kuwa na matumizi mengine, cha msingi ni kutambua uwezo wa hiyo taka katika kukusaidia katika mahitaji yako mbalimbali.

BADILI TAKA KUWA BIDHAA ITAKAYO KUFAA NA KUTENGENEZA NISHATI

Kuna baadhi ya taka zinaweza kubadilishwa katika mazingira ya nyumbani kuwa bidhaa yenye tija; lakini kuna baadhi ya taka kama vile plastiki zinahitaji mazingira ya kiwanda ili kubadilishwa.

  • Taka zenye asili ya metali kama vile nyaya, vifaa vya kielekroniki, magari, baiskeli n.k. vinaweza kuuzwa katika meneo ya kukusanyia vyuma ili vije kubadilishwa kuwa bidhaa nyingine. Baadhi ya vitu kama vile simu mbovu huweza kuuzwa kwa mafundi wa simu ili vifaa vyake vipate kutumika kwajili ya shughuli nyingine.
  • Taka zenye asili ya plastiki zinaweza kukusanywa na kuuzwa katika makusanyo ya taka za plastiki ili zipate kubadilishwa na kuwa bidhaa nyingine za plastiki. Kwa hili pia siku hizi tumeona jinsi ambavyo limekuwa ajira kwa watu wengi.

Nishati inaweza kutengenezwa kutoka katika baadhi ya taka, hivyo huweza kusaidia kupunguza kiasi cha takataka pamoja na kuleta tija ya kinishati. Kutengeneza nishati kutokana na taka  mara nyingi kumekuwa kukisaidia pia kupunguza athali ya taka kwa mazingira na afya.

  • Kinyesi na mkojo vyaweza kutumika kutengenezea umeme na kupata gesi. Aina hii ya gesi hutokana na kuoza kwa taka zenye asili ya kaboni. Gesi hii inapochukuliwa vizuri huweza kutupa chanzo mbadala cha umeme na gesi ya kupikia. Mfumo huu unaweza kufungwa kitaalamu katika majumba yetu ili mradi ufuate taratibu na sheria.
  • Baadhi ya taka ngumu kama vile miti, mbao, karatasi huweza kutumika kuzalisha nishati. Hii mara nyingi imekuwa ikifanyika katika maeneo mengi. Katika shughuli za kuteketeza takataka, joto linalotengenezwa huweza kutumika tena kwajili ya shughuli nyingine za maendeleo.

TUPA TAKATAKA

Hii ni hatua ambayo ni ya mwisho katika kudhibiti taka. Utupaji taka ufanyike baada ya taratibu nyingine za kudhibiti taka kufanyika ikiwa ina maana ya kwamba iwe kwa namna fulani kabisa mmeona hamuwezi kuzitumia tena hizo taka. Utupaji taka uwe ni hatua ambayo imeonekana kabisa kwamba kutupa taka ni faida kabisa kuliko kubaki nazo. Swala la kutupa takataka linapaswa kufanyika katika uangalifu ili lihifadhi mazingira na afya. Utupaji taka hujumuisha maji-taka na taka-ngumu.

  • Kuna mifumo ya kitaalamu ya kutupa maji-taka ambayo mingine tumekuwa tukiitumia kama vile mashimo ya maji machafu, mifereji ya maji machafu. Sheria na taratibu za kitaalamu zifuatwe huku swala zima la afya na mazingira vikipewa kipaumbele.
  • Utupaji wa taka ngumu huweza kufanyika kwa namna nyingi pia. Taka zinaweza kuchomwa moto, kuwekwa katika maeneo maalumu ya wazi au kufukiwa ardhini. Maeneo mengi ya nchi za wenzetu, taka ngumu za nyumbani zimekuwa zikikusanywa kwa pamoja kwa kutumia magari maalumu kisha hupelekwa na kuwekwa sehemu moja kwajili ya kuzichambua kisha baadhi kuzitupa kwa kuzichoma moto, kuzifukia au kuziweka katika maeneo maalumu ya wazi.

Mwisho katika maada yetu ya kudhibiti taka katika nyumba zetu, ni muhimu kukumbuka kuwa taka sio taka ikimaanisha kwamba waweza kuzitumia taka kwa manufaa zaidi. Taka zimekuwa taka kwasababu mtu huyo ameona hazimfai kwa muda huo, ijapokuwa mwingine zinaweza kuwa kitu chenye thamani kwake. Ni muhimu udhibiti taka ufanyike katika utashi wa kulinda afya na kuhifadhi mazingira. Jaribu kuzipa taka matumizi mbadala yenye tija kwako, na swala la kuzitupa liwe la mwisho kabisa. Wapo wataalamu wengi katika nchi yetu ambao wanaweza kukupa huduma ya kuwa na mfumo mzuri katika nyumba yako wa kudhibiti taka, kinacho hitajika ni nia ya dhati.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TZ
From TZS 100,000/day
Kinondoni
10 years
Mtaalamu wa mambo ya ujenzi wa makazi aliyesomea na mwenye uzoefu wa muda mrefu, kutoka kwenye kusanifu ramani za nyumba, usanifu wa nadharia ya nje ya nyumba na bustani, pamoja na mambo ya makisio na mahesabu ya gharama za ujenzi. Lengo letu ni kukuwezesha kutimiza nyumba ya ndoto yako sasa, bila kujalisha kama ni ya gharama nafuu au mjengo wa heshima.
3D Rendering Building Designing Cost Estimation Landscape Designing Project Management Project Planning Technical Drafting

14_Photo – 24f

ID-20968
4
275 sqm
189 Pcs
19 m
4,923 Pcs
18 m
2,448 Pcs

C1_Photo – 23

ID-16471
4
190 sqm
134 Pcs
15 m
3,491 Pcs
14 m
1,736 Pcs

NXL 18 – 1

ID-18239
3
238 sqm
0 Pcs
13 m
6,919 Pcs
12 m
1,756 Pcs

IMG-20220722-WA0034

ID-28239
3
168 sqm
115 Pcs
14 m
3,001 Pcs
14 m
1,492 Pcs

BROWN 2BHK_Photo – 42

ID-13471
2
72 sqm
61 Pcs
10 m
1,389 Pcs
8 m
514 Pcs

POST 56 – 0-2

ID-17679
3
212 sqm
88 Pcs
14 m
6,086 Pcs
13 m
2,630 Pcs

517780131152825596171742858392522750887936n

ID-15415
4
278 sqm
0 Pcs
18 m
9,043 Pcs
18 m
2,450 Pcs

67526197_219861218992137_4358816373125664861_n

ID-16975
2
113 sqm
46 Pcs
13 m
2,713 Pcs
12 m
1,006 Pcs

DDDDD_Photo – 30

ID-16503
4
235 sqm
162 Pcs
17 m
4,207 Pcs
16 m
2,092 Pcs

HUM_Photo – 51A

ID-29203
2
123 sqm
85 Pcs
15 m
2,210 Pcs
8 m
1,099 Pcs

NXL-26-1

ID-17177
4
244 sqm
124 Pcs
13 m
4,000 Pcs
12 m
1,902 Pcs

POST 69 – 2

ID-17630
4
194 sqm
133 Pcs
17 m
3,473 Pcs
14 m
1,727 Pcs

Join Membership

Join our membership to become a part of our expansive platform dedicated to residential development in Africa. Gain access to house plans, informative articles, vetted builders, plot listings and construction materials!

Eng. Lwifunyo Mangula
Payment Challenges? WhatsApp Admin