Njia 3 mahususi za kupata mtaji wa kujengea nyumba yako
Kuna njia nyingi za kupata mitaji ya ujenzi, hapa chini tumezichambua katika makundi makuu 3 ambayo yanaweza kukusaidia kujenga mtazamo wa namna ya kuweza kukamilisha mtaji wa kujengea nyumba yako. Mwisho wa siku utaweza jua ni ipi ambayo inakufaa zaidi kwako binafsi. Tumia Pesa yako binafsi uliyo nayo Kujenga yote kwa pamoja Kujenga kidogo kidogo […]
Kazi ya linta katika jengo
Linta ni moja ya kiungo katika jengo ambacho huwekwa juu ya sehemu zilizo achwa wazi katika kuta za jengo ili kubeba mzigo juu yake na kuupeleka salama mpaka katika maegemeo; ni kiungo kinachowekwa juu ya uwazi wa madirisha, milango, mageti n.k ili kuweza kubeba mzigo juu yake bila kunepa. Kiungo hiki ni muhimu kwani uwazi […]
Kazi ya msingi katika nyumba
Msingi ni sehemu muhimu ya jengo ambayo huunganisha jengo na ardhi husika pamoja na kupeleka mzigo wa jengo kwa usalama kabisa katika ardhi. Pasipo msingi, jengo linakuwa halijakamilika na halipo salama. Kikawaida msingi hutumia gharama kubwa katika kujenga ukilinganisha na baadhi ya maeneo katika jengo, gharama hii kubwa inaashiria umuhimu na ulazima wa sehemu hii ya jengo.