Sebule kwa kawaida ni sehemu ya ndani ya nyumba ambayo ni maalumu kwa kupumzikia, kujumuika na kupokelea wageni.  Kuna muingiliano wa maneno haya living room – sitting room – lounge – lounge room – front room kutegemea na eneo na mabadiliko ya kitamaduni. Maana ya sebule mimi binafsi nimeiona ipo katika KUPUMZIKA, KUJUMUIKA na KUPOKEA WAGENI.  Sebule sio chumba tu cha kawaida, ni sehemu yenye sifa zake muhimu! Je, sebule yako ina hizo sifa 3?

Sifa hizo tatu za sebule zimebebwa katika mambo mawili ya kitaalamu. Hivyo unapo andaa sebule yako kabla ya kuijenga ni lazima hivi vitu viwili viaangaliwe kwa umakini. Vitu hivyo ni

Mpangilio na Upande ilipowekwa kuhusiana na nyumba

Mandhari/ Usanifu wa ndani wa hicho chumba

Rangi, mwanga, unyororo, mpangilio, mpishano, kimo, mfanano, ukubwa, umbile la Sebule na vitu vyake huathiri hali za watumiaji. Mpangilio wa vitu sebuleni huleta ladha fulani.

Mpangilio wa vitu na samani mbalimbali katika sebule unaleta ladha fulani! Maumbo ya hivyo vitu hubeba maana fulani na kuathiri hali za watumiaji. Ni muhimu kuchagua vitu vyenye kuleta ladha nzuri unayotaka katika sebule yako! Kutochagua hali unayoitaka katika sebule yako ni kumaanisha kuwa unaruhusu hali yeyote ile kuathiri watumiaji wa sebule yako, ambayo inaweza kuwa hali nzuri au mbaya! Amua sasa ni hali gani unataka iathiri watumiaji wa sebule yako!

Mambo machache kuhusu rangi; rangi zinaweza sababisha hisia ya utofauti kwa binadamu na wanyama mbalimbali. Kwa hiyo unachagua rangi ya kutumia kulingana na aina gani ya uhali ambao unataka kuutengeneza katika chumba chako!

Unaweza kujiuliza, Kwanini alama za barabarani zina rangi ya njano/nyeupe kwa nyeusi? Rangi huathiri watoto, wazee, wageni n.k. Inaweza leta uchangamfu, uhuru, hofu n.k.

Msukumo hafifu wa rangi upo katika bluu, urujuani (rangi za ubaridi). Rangi zenye msukumo hafifu ni nzuri hata kupaka katika eneo kubwa. Ndio maaana rangi za njee za nyumba kama vile light blue hutumika kupaka nyumba. Fikili ingekuwa vipi nyumba ingepakwa rangi nyekundu tii!

Rangi zenye msukumo wa nguvu ni kama nyekundu, machungwa (orange), zambarau (purple) (rangi za ujoto). Pia rangi inaweza kuwa ina ugiza au mg’ao. Rangi zenye ubaridi na ugiza zikipakwa juu kama dari huweza leta hisia za kutisha (threatening).

Rangi nyeupe ni neutral, nyeupe huweza leta hisia za usafi, takasa, utaratibu. Rangi Nyeupe huendana na rangi mbalimbali.

Mtu fulani alijaribu kuonesha hali na athari mbalimbali zinazotokana na rangi; Usitumie hivihivi, zinahitaji utaalamu maalumu katika kutumia.

Haya chini ni mapendekezo ya wataalamu fulani kuhusiana na rangi ambayo unaweza kupaka katika vyumba vya nyumba yako. Tumia wataalamu ili wakushauri namna ya kuzitumia ili utengeneze ladha nzuri

Tumia samani, kuta, mimea maalumu, mapazia n.k katika kubeba rangi ambazo umekusudia.

Ni vyema kutengeneza sebule yako katika uzuri wake huku ukikumbuka kuwa sebule ni sehemu ya kupokelea wageni, kupumzikia na kujumuikia. Usisite kuwasiliana na wataalamu wako ili wapate kukusaidia kupata sebule yenye ubora wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *