Namna ya kujenga na kurekebisha kuvuja paa kwa nyumba za contemporary (zilizofichwa paa/ hidden roof)
Nyumba za contemporary au hidden roofing zimekuwa ni moja ya staili ya nyumba ambazo watu wengi kwa sasa wanapenda kuzijenga haswa vijana maana ndizo zilizo za ‘kisasa’ kwa sasa! Nyumba hizi zimekuwa zinavutia watu wengi sababu ya mwonekano wake wa boksi, ubapa na kona nzuri zilizoibeba nyumba na kuifanya kuvutia. Uzuri wake ni rahisi sana […]
Kazi ya linta katika jengo
Linta ni moja ya kiungo katika jengo ambacho huwekwa juu ya sehemu zilizo achwa wazi katika kuta za jengo ili kubeba mzigo juu yake na kuupeleka salama mpaka katika maegemeo; ni kiungo kinachowekwa juu ya uwazi wa madirisha, milango, mageti n.k ili kuweza kubeba mzigo juu yake bila kunepa. Kiungo hiki ni muhimu kwani uwazi […]
Kazi ya msingi katika nyumba
Msingi ni sehemu muhimu ya jengo ambayo huunganisha jengo na ardhi husika pamoja na kupeleka mzigo wa jengo kwa usalama kabisa katika ardhi. Pasipo msingi, jengo linakuwa halijakamilika na halipo salama. Kikawaida msingi hutumia gharama kubwa katika kujenga ukilinganisha na baadhi ya maeneo katika jengo, gharama hii kubwa inaashiria umuhimu na ulazima wa sehemu hii ya jengo.
TATIZO LA NYUFA KATIKA NYUMBA YAKO
Kuna sababu nyingi za nyufa katika nyumba zetu za makazi; kwa ujumla vinyufa vyembamba katika kuta, dari, lipu n.k inaweza kuwa ni alama ya kusinyaa na kutanuka kwa sehemu mbalimbali katika nyumba yako ambako kwaweza kuwa kunasababishwa na unyevunyevu, joto, mabadiliko ya kikemikali katika vifaa vilivyotumika kujengea nyumba (rangi, maji, cement, nondo…) ambayo husababisha kusinyaa […]