Namna ya kujenga na kurekebisha kuvuja paa kwa nyumba za contemporary (zilizofichwa paa/ hidden roof)

Nyumba za contemporary au hidden roofing zimekuwa ni moja ya staili ya nyumba ambazo watu wengi kwa sasa wanapenda kuzijenga haswa vijana maana ndizo zilizo za ‘kisasa’ kwa sasa! Nyumba hizi zimekuwa zinavutia watu wengi sababu ya mwonekano wake wa boksi, ubapa na kona nzuri zilizoibeba nyumba na kuifanya kuvutia. Uzuri wake ni rahisi sana kuuona ukilinganisha na nyumba za staili ya kawaida  (classical style).

Makazi Team  |  +255-657-685-268

Ijapokuwa nyumba hizi ni nzuri na zimekuwa zinavutia watu wengi sana, bado kumekuwa na malalamiko na woga wa kuvuja ktk nyumba hizi maana wengi ya waliozijenga wamekuwa wakilalamika kuvuja kwa paa; Ni kweli wapo baadhi ya wamiliki ambao nyumba zao zimekuwa zikivuja ambapo sababu haswa ya kuvuja imekuwa ni kukosea kuzijenga vile inavyotakiwa. Maji lazima yawekewe njia sahihi ya kushuka chini vyema bila kuchepuka. Kushindwa kujenga kwa nyumba hizi ni kutokana na kukosa wataalamu sahihi wa kuandaa michoro ya kitaalamu (ramani) inavyotakiwa kwa nyumba hizi ambayo inayoelekeza nyumba na mfumo mzima wa paa ukaaje ili lifanye kazi vyema. Pia sababu ya pili ni kukosa mafundi sahihi wanaojua namna ya kuzijenga nyumba hzi haswa ktk mfumo wa paa la staili hii; wengi wa mafundi wamekuwa hawajui namna sahihi ya kujenga mfumo wa paa wa nyumba hizi sababu wanatumia uzoefu tuu bila kutafuta kujifunza namna sahihi ya kuzijenga nyumba hizi. Kumbuka tunazungumzia nyumba za contemporary/zilizoficwa bati ambazo zimeezekwa bati.

Mambo muhimu ya kuvingatia ktk ujenzi wa mfumo wa paa la contemporary

  • MWINUKO WA PAA
    • Ni muihimu kuhakikisha paa lako limeinuka vya kutosha kuhakikisha kuwa maji yako yanatiririka vyema kwenda chini. Swala la mwinuko wa bati linategemea aina ya bati na umbali maji yanasafiri ktk bati.
    • Maji kama yanasafiri umbali mrefu mpaka yatoke ktk bati basi mwinuko wa paa unapaswa kuwa juu zaidi. Kila mzalishaji wa bati huelekeza mwinuko wa bati inabidi usipungue kiasi gani; ambapo kama mwinuko ni mdogo basi maji yatatiririka polepole na kupenya ktk maungio na kulowesha nyumba; na pia mwinuko mdogo unaweza pelekea bati kupata kutu na kuoza haraka sababu maji yanapata muda wa kukaa ktk bati na kuliozesha.
    • Utatuzi kuvuja paa:
      • kama umegundua paa lako lina mwinuko mdogo ukilinganisha na maelekezo ambayo umepewa na mzalishaji wako wa bati ulizotumia, basi waweza kufanya mambo mawili
        • Kuongeza mwinuko wa paa lako kwa kurekebisha kenchi zako; hatua hii itahitaji ufumue kenchi na bati zako na upige upya
        • Kubadili aina ya bati na uweke aina nyingine ambazo zinakidhi mwinuko uliopo wa paa lako bila kubadili kenchi
      • kwa ambate hujaanza kujenga nyumba yako, basi hakikisha paa lako limeinuka vyema na kukidhi kiwango ambacho mzalishaji wako wa bati amekupa

 

  • MPANGILIO WA PAA
    • Ni muhimu kutumia wataalamu waliosomea na wenye uzoefu na mambo ya ujenzi wa nyumba ili uweze kuandaliwa ramani yako ambayo itamwongoza fundi wako aweze kujenga nyumba vyema inavyotakiwa. Nyumba yako inavyosanifiwa basi ni muhimu paa lake liwe rahisi(simple) kulipangilia na kushusha maji kwa haraka. Jitahidi kuepuka mapaa ambayo yanakona kona nyingi, yana shusha maji kwenda ktk bati jingine badala ya kwenda ktk gutter, paa lenye kumwaga maji pande mbalimbali. Jitahidi paa lako liwe na mwonekano rahisi ambao pia hata ujengaji wake uwe rahisi. Epuka paa gumu ambalo pia litampa ugumu fundi wako kulielewa na pia kulijenga. Paa lako liwe na mwelekeo wa maji moja kwa moja kwenda ktk gutter; epuka kuwa na gutter nyingi, moja au mbili zinatosha.
    • Utatuzi kuvuja paa:
      • kama unaona kuvuja kwa paa lako kunatokana na mpangilio mbaya wa paa basi hakikisha unatafuta mtaalamu wa ramani mzuri aje rudia kusanifu paa lako liwe rahisi kujenga kisha tafuta fundi mzuri wa paa anayejua kujenga hizi nyumba arudie kupiga paa huku akisimamiwa na mtaalamu wa ramani aliye fanya marekebisho hayo.
      • Pia kama hujaanza kujenga na ukaona ramani yako paa lake limewekwa gumu (complex), basi tafuta mtaalamu wa ramani mzuri aweze fanya marekebisho wa ramani yako haswa upande wa paa liwe rahisi.

 

  • MAJI YAPEWE MWELEKEO WAKE
    • Maji yasipotengenezewa njia basi huwa na tabia ya kutengeneza njia yake yenyewe ambapo yanaweza tengeneza njia ambayo italeta matatizo ktk nyumba yako. Maji yote ya mvua yanayoshuka ktk paa lako hakikisha yanapewa mwelekeo ulio rahisi mpaka yafike chini; yaani yanaposhuka ktk bati yapokelewe na kuelekezwa upande wa kwenda kwa ulalo wa bati na kisha yasafiri kwenda kwenye gutter. Yakipokelewa ktk gutter yatiririshwe vyema kwenda ktk downpipe moja kwa moja mpaka chini (au ktk tanki la kuhifadhia maji); hakikisha maji hayatuami ktk gutter bali yanaelekezwa kwenda ktk downpipe vyema kwa ulalo wa gutter lako kiasi.
    • Utatuzi kuvuja paa:
      • Kama umegundua kuvuja kwa paa lako kunatokana na maji kutokuwa na mwelekeo mzuri ulioandaliwa kuelekea, basi tafuta mtaalamu mzuri wa ramani aje aangalie nyumba yako kisha aweze sanifu paa lenye kuelekeza maji yaelekee wapi kwa urahisi. Kisha tafuta fundi mzuri ya paa za contemporary aje atoe hilo paa na kujenga jingine jipya lililo bora lenye kuelekeza maji vyema kwa urahisi huku akisimamiwa na mtaalamu aliyeandaa ramani hiyo mpya.
      • Pia kama umegundua ramani yako ya nyumba haina paa lenye kuelekeza maji vyema namna ya kwenda, basi tafuta mtaalamu wa ramani mzuri arekebishe ramani yako

 

  • GUTTER
    • Gutter ni moja ya sehemu muhimu ya paa ktk nyumba hizi za contemporary; Gutter ndilo lenye kupokea maji yanayotoka ktk bati na kuyakusanya na kuyapeleka ktk downpipe chini. Kwa nyumba za contemporary mara nyingi gutter lake linajengwa kwa zege. Ni muhimu kuhakikisha gutter lako ni kubwa kwa upana na kimo ili liweze kuyakusanya maji yooote ya paa bila kulemewa maana kama likilemewa kwa wingi wa maji basi litaanza kuvujisha maji kwenye nyumba. Jenga gutter kwa kutumia materials ambayo yanazuia kuvuja gutter ktk kipindi chote cha uhai wa nyumba. Mambo ya kuzingatia ktk gutter
      • Liwe na kimo na upana mkubwa kukusanya maji yote bila kulemewa au kufurika. Ukubwa wa gutter unategemea na kiasi cha maji kutoka ktk paa kwenda ktk gutter. Gutter yako iwe pana ambayo itaruhusu watu kupata nafasi wakati wa kuijenga na kuisafisha.
      • Tumia zege yenye kupigwa vibration; tumia Water proof cement kujengea
      • Piga water proofing membrane ktk gutter yote vyema ili maji yasipenye ktk zege; Epuka kutumia marumaru kama water proofing maana huvujisha pia.
      • Gutter liwe na uimara kuweza kujibeba na kubeba maji yote bila kuvunjika au kupinda. Hakikisha gutter limekaa ktk kuta au nguzo vyema na kuimarishwa na nondo
      • Hakikisha gutter lako linatirisha maji kuelelea ktk downpipe ili maji yasituame ktk gutter. Hakikisha gutter lako lipo smooth ktk mfereji wa ndani ili maji yasipate mpenyo au kuozesha gutter na yawe yanatereza tuu
    • Utatuzi kuvuja paa:
      • Kama kuvuja kwa paa lako kupo ktk gutter au kunatokana na ubovu wa gutter, basi hakikisha unatatua tatizo hilo. Kama gutter linafurika maji au kwamba ni dogo kupokea maji mengi, basi panua ukubwa wa gutter. Kama gutter linavuja au maji yanapenya ktk gutter au kuna matone yanamwagika kupitia gutter basi tafuta fundi wa water proofing aweze kupiga gutter yako water proof materials yenye kuzuia maji kupenya. Kama gutter lako linatuamisha maji basi hakikisha gutter lako unaliweka smooth na pia liwe na muinamo kidogo kufanya maji kutiririka kwenda ktk downpipe na downpipe ziwe kubwa na nyingi za kutosha kushusha maji yote chini.
      • Kama ramani yako umegundua haijakaa vyema ktk gutter na inaweza leta changamoto za kuvuja basi hakikisha unatafuta mtaalamu wa ramani aweze rekebisha hilo

 

  • DOWNPIPE
    • Downpipe ni bomba ambalo linashusha maji chini kwa kuyapokea kutoka ktk gutter na kuyapeleka chini ardhini au ktk mfereji au tanki la kuhifadhia maji. Ni muhimu kuhakikisha kuwa kila gutter ina downpipe na pia ziwe za kutosha kushusha maji bila kufurika. Maji yasisafiri umbali mrefu bila kufikia downpipe. Kama downpipe ni ya zege au tofali basi hakikisha imejengwa kwa water cement na kuwa treated na water proofing membrane ili isivuje. Kama unatumia downpipe ya plastiki au bati basi hakikisha inakuwa na ukubwa wa kutosha na pia itaweza dumu kwa kipindi choto ch uhai wa nyumba. Weka chujio juu ya downpipe ili uchafu usipenye na kuiziba
    • Utatuzi kuvuja paa:
      • Kama kuvuja kwa paa lako kunatokana na ubovu wa downpipe basi hakikisha unatatua. Kama maji yanatuama ktk gutter kutokana na kuwepo kwa downpipe chache au ndogo basi ongeza idadi ya downpipe sehemu mbalimbali za gutter na pia ziwe na ukubwa wa kutosha. Kama downpipe zako zimeziba basi zizibue na kisha weka chujio juu ya downpipe. Kama kuta za nyumba zinalowa kutokana kuvuja downpipe, basi waweza badili downpipe uweke ambazo hazivuji au pigeni water proofing ktk downpipe hizo vyema toka ktk maungio na gutter mpaka chini.
      • Pitia ramani yako kama hujaijenga uweze ona kama downpipe zipo za kutosha na zenye kiwango ambazo hazitaleta tatizo la kuvuja

 

  • MAJI BAADA YA DOWNPIPE
    • Ni muhimu kuhakikisha kuwa maji yakitoka ktk downpipe yanapelekwa sehemu iliyo sahihi. Inawezekana paa lisivuje, ila maji yanayotoka ktk paa kama hayapewi mwelekeo sahihi wa kwenda yanaweza leta matatizo sehemu nyingine za nyumba; maji yanaweza fumua msingi au kufurika na kuingia ndani; pia maji yanaweza leta mmomonyoko wa ardhi kama hayata dhibitiwa vyema. waweza vuna maji yanayotoka ktk paa na yakatumika kwa matumizi mengine kama usafi, umwagiliaji, kilimo hadi kupikia kama yatatibiwa vyema.
    • Utatuzi kuvuja paa:
      • Je, maji yanayotoka ktk downpipe yanaleta athari ktk nyumba yako? Basi yatafutie njia ya kwenda vyema bila kuharibu nyumba au mazingira.; pia waweza fanya uvunaji wa maji hayo ya mvua na yakakusaidia ktk matumizi mbalimbali
      • angalia pia ktk ramani ya nyumba yako kama mmepangilia vyema kuwa maji ya kutoka ktk downpipe yatakwenda wapi; kama unaona yanapokwenda yataleta athari ktk nyumba basi chukua hatua kurekebisha kabla ya kujenga; fikiri kuyafanyia uvunaji maji hayo ili uyatumie kwa shughuli nyingine

 

  • MAUNGIO YA BATI, GUTTER, DOWNPIPE NA KUTA
    • Moja ya sehemu ambazo zimekuwa zinavuja sana ni ktk maungio ya bati na bati, bati na kuta, kuta na gutter, gutter na downpipe… ni muhimu kuhakikisha maungio haya unayadhibiti vyema ili yasiweze kuvuja. Kama ktk maungio ya bati na kuta hayajakaa vyema, basi kuna uwezekano kuwa maji yakapenya au kumfyonzwa ukutani na kupelekea kuvuja au unyevunyevu ktk kuta. Hakikisha mpangilio wa bati na kuta unawekwa vyema ili maji yasipate nafasi ya kupata mpenyo. Waweza tumia waterproofing kufunika maungio hayo vyema ili yasivuje; pia waweza tumia viungo vilivyoandaliwa maalumu kuunganisha maeneo hayo ambavyo havivujishi
    • Utatuzi kuvuja paa:
      • Kama maungio ya gutter na bati yanavuja basi kwanza angalia sababu ya kuvuja zaidi inatokana na nini; waweza tumia water proofing kufunika maungio hayo pia. Angalia namna nzuri ya kuyaelekeza maji kutoka ktk kuta kuja ktk bati na katika bati kwenda ktk gutter na yawe kinamna ambayo hayapati mpenyo wa kuvuja.
      • Kama jengo ambalo unataka kuanza kujenga bado hujawa na uhakika vyema namna gani maungio yake ya paa yatakaa, basi rudia kupitia na kurekebisha tena michoro yako ili kuhakikisha maungio hayavuji

 

  • AINA YA BATI
    • Maji ktk paa yanaweza kuvuja kutokana na aina ya bati; Kama umetumia bati ambazo umeunganisha vipande vipande kabla ya maji kufika chini ktk gutter, basi kuna hatari ya kuweza kuvuja kama hakutakuwa na umakini, hivyo tunashauri utumie bati ndefu moja toka juu mpaka chini kwenda ktk gutter ili kuepuka hatari ya kuvuja. Nenda kiwandani halafu agiza bati ambazo ni ndefu moja kwa moja kulingana na jengo lako lilivyo
    • Pia ni muhimu kuhakikisha unatumia material ya bati ambayo unajua hata kama bati litainuka kidogo na maji kutiririka polepole basi bati lako halitaharibika au kuoza ktk kipindi cha uhai wa nyumba. Maungio/overlaping ya bati moja na jingine weka ya kutosha ambayo itahakikisha kuwa maji hayapati nafasi ya kupenya maana ktk contemporary houses paa haliinuki sana hivyo inaweza yapa maji muda wa kupenya ktk maungio. Tumia bati ambazo gauge yake ni ngumu kupinda.
    • Ktk bati pia hakikisha kuwa umbali kati ya mbao na mbao unakuwa ule unaotakiwa ili bati zisipinde, yaani purlins. Na pia nashauri tumia rangi ya bati ambazo zinaakisi joto zaidi ili kupunguza ndani ya paa kusiwe na joto sana. Bati zilizolala sana kimwinuko zina hatari ya kupinda na kuacha mwanya wa maji kupenya pale ambapo watu wanapopita juu yake, hivyo ni muhimu nafasi kati ya mbao purlins ziwe jirani jirani zaidi ili watu waweze kanyaga humo na pia kupunguza hatari ya kupinda bati
    • Misumari ambayo utaitumia basi hakikisha haiachi matobo ktk bati; kuwa makini ktk kupiga misumari ktk bati na isiache matobo au mwanya wa maji kupita. Tumia misumari yenye kofia yenye mpira ambao utabana vizuri bati na lisivuje.
    • Hakikisha unanunua bati na vifaa vyote vya paa vyenye kiwango kinachokubalika kitaalamu kulingana na hali yako ya paa.
    • Utatuzi kuvuja paa:
      • Kama kuvuja ktk nyumba yako kunatokana na aina ya bati au namna ambavyo bati zimepigwa, basi angalia namna ya kurekebisha tatizo hilo. Kama bati zimepinda kutokana na watu walivyopita juu, basi waweza ziondoa hizo bati na kisha ukarekebisha nafasi kati ya mbao na mbao (purlins) iwe ndogo zaidi kulingana na kiwango cha kitaalamu; pia badili bati na tumia zile zenye gauge iliyo ngumu zaidi kupinda. Kama bati zako zimeoza au kupata kutu basi angalia namna ya kubadili kati ya bati na utumie zenye materials ambayo hayaozi kulingana na hali ya paa lako au ongeza mwinuko wa paa lako ili maji yapate kutiririka haraka kwenda chini; pia tumia bati ambazo zimepakwa rangi kutoka kiwandani. Kama ktk misumari kuna kuvuja au kuna matobo basi tumia silikoni au waterproofing kuziba matobo hayo vyema.
      • Kama ndio unapanga kuanza ujenzi mpya kabisa, basi hakikisha unatumia vifaa vyenye kiwango cha kitaalamu kulingana na hali yako ya paa. Hakikisha kuwa unatumia misumari yenye vipira ktk kofia, tumia bati ndefu moja kwa moja, tumia bati zilizo ngumu na za rangi. Overlaping/maungio ya bati na bati hakikisha yanakuwa yana ukubwa wa kutosha ili kuzuia maji kupenya na kuvuja

 

  • NJIA YA KUPANDA KWENDA JUU YA PAA
    • Hili na jambo la muhimu kuweza kuliangalia, maana tumeona kuwa moja ya sababu ya kuvuja paa ni kupinda kwa bati pale watu wanapozikanyaga; hivyo ni muhimu kuamua upandaji wa watu juu kwenda ktk paa. Kwanza sishauri watu wapande juu ktk paa kama si kwa sababu maalumu haswa ya kiufundi. Hivyo basi hatushauri kuweka ngazi za kudumu kwenda juu ktk paa ili tusiweke mlango wa kudumu kwenda ktk paa; kama ni fundi basi atatafuta ngazi ya muda na aiweke ili aweza kupanda kwenda juu ktk paa. Katika paa ni muhimu kuwe kuna kinjia au kisehemu ambacho watu wanaweza pita bila kukanyaga bati ili kuzuia kupinda kwa bati; unaweza weka upana wa gutter mkubwa ili hata watu wawe wanaweza pita humo ktk gutter. Pia waweza weka katazo na maelekezo ya namna ya kupanda juu ktk paa ili kuepuka hatari ya kupindisha bati au matatizo juu ya paa. Pia angalia kuwe na namna ya kuweza kusafisha gutter na downpipe vyema bila kuharibu paa lako.
    • Utatuzi kuvuja paa:
      • Kama kuvuja kwa paa lako kunatokana na watu kupanda juu ktk paa na kupindisha bati, basi fanya hatua ya kuzuia watu kupanda juu ktk paa; pia hakikisha unaweka ‘njia maalumu’ ya watu kuweza kupanda juu bila kukanyaga bati ili kuepuka kupinda kwa bati zako na kisha kuvuja.
      • Je, umehakikisha nyumba yako unayopanga kuijenga ina namna nzuri ya kuzuia watu kupanda juu ktk paa ili kuepusha hatari ya kupindisha bati? Kumbuka pia kuweka namna nzuri ya kusafisha paa lako ambayo haitasababisha watu kuharibu bati zako.

 

Hivyo basi, inahitajika umakini na utaalamu ktk kujenga mfumo wa paa wa nyumba za contemporary/ paa lililofichwa ili kuhakikisha unaifurahia nyumba yako vyema ktk kipindi chote cha uhai wa nyumba. Hakikisha unakuwa makini kutumia wataalamu wenye weledi na ubora wa kazi tangu katika usanifu wa nyumba hadi ujenzi ili kuepuka gharama za baadaye za kuja kufanya marekebisho.

Kwa mtu ambaye anaona kuna tatizo la kuvuja ktk paa la nyumba yake ya contemporary, basi tafuta wataalamu waweze kukusaidia kugundua tatizo haswa ni lipo na kisha kurekebisha vyema tatizo la kuvuja. Nyumba za contemporary ni nzuri na kuvutia na haziwezi kuwa na tatizo la kuvuja kama zitajengwa kwa kufuata mwangaza wa kitaalamu.

Makazi Team

www.makazi.network

+255-657-685-268

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ID-27395
4
271 sqm
182 Pcs
19 m
4,726 Pcs
17 m
2,350 Pcs
ID-10129
3
100 sqm
33 Pcs
12 m
2,024 Pcs
10 m
890 Pcs
ID-11264
1
32 sqm
25 Pcs
7 m
698 Pcs
6 m
313 Pcs
ID-13362
4
243 sqm
136 Pcs
21 m
4,072 Pcs
15 m
2,059 Pcs
ID-17034
5
222 sqm
135 Pcs
15 m
4,168 Pcs
13 m
1,775 Pcs
ID-19343
3
155 sqm
107 Pcs
14 m
2,775 Pcs
14 m
1,380 Pcs
ID-27923
4
162 sqm
110 Pcs
15 m
2,899 Pcs
14 m
1,440 Pcs
ID-18248
4
396 sqm
0 Pcs
18 m
12,252 Pcs
12 m
3,069 Pcs
ID-22351
2
51 sqm
46 Pcs
8 m
785 Pcs
8 m
420 Pcs
ID-19790
4
240 sqm
99 Pcs
19 m
5,760 Pcs
16 m
2,136 Pcs
ID-11075
4
175 sqm
77 Pcs
11 m
4,683 Pcs
10 m
901 Pcs
ID-17116
3
144 sqm
99 Pcs
13 m
2,578 Pcs
13 m
1,282 Pcs
Makazi Icon Blue

Join Membership

Join Membership to See Clear Floor Plans Before You Buy the Full Plan; See How Much MONEY is Needed to INVEST in Your Business In order to Get the Profit to Finance Construction of This House. What MORTGAGE to Borrow and Return Monthly to Your Bank. Also, See How Much it COSTS to Build the Foundation, Walling, Roofing, Ceiling, Painting, Doors, Windows… in All of Our Houses on This Platform so That You Can CHOOSE, COMPARE, PLAN & STRATEGIES on How to Approach Your Construction Rightly!