TATIZO LA NYUFA KATIKA NYUMBA YAKO

Kuna sababu nyingi za nyufa katika nyumba zetu za makazi; kwa ujumla vinyufa vyembamba katika kuta, dari, lipu n.k inaweza kuwa ni alama ya kusinyaa na kutanuka kwa sehemu mbalimbali katika nyumba yako ambako kwaweza kuwa kunasababishwa na unyevunyevu, joto, mabadiliko ya kikemikali katika vifaa vilivyotumika kujengea nyumba (rangi, maji, cement, nondo…) ambayo husababisha kusinyaa na kutanuka. Maeneo kama ya jikoni, bafuni huweza kukumbwa na nyufa ndogondogo kutokana na maji na joto ambavyo vikaathiri ukuta wako. Mbao huweza kusinyaa na kutanuka kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa ya kiunyevunyevu na joto. Jengo ambalo lipo jirani na barabara yenye shughuli nyingi huweza kuathirika na nyufa kutokana na mitikisiko mbalimbali.

Nyufa nyembamba mara nyingi huathiri mwonekano wa jengo lako zaidi ya uimara. Ijapokuwa nyufa nyembamba zaweza kuja kusababisha nyufa kubwa na kisha kuleta madhara makubwa; ni vyema kuzitafutia ufumbuzi aina hii ya nyufa ili kuhakikisha uimara na afya ya jengo.

Nyufa kubwa katika nyumba huweza kutokana na matatizo mbalimbali katika jengo lako; matatizo katika msingi, hali ya udongo, kuzidiwa mzigo n.k huweza kusababisha jengo lako kupata nyufa ambazo zikaathiri afya ya jengo na watumiaji. Tutaangalia baadhi ya vipengere vya muhimu katika aina hizi za nyufa kubwa ili tuweze kupata mwanga katika ujenzi na uwekezaji wetu.

Nyufa katika msingi

Nyufa katika msingi mara nyingi zinatokana na matatizo katika udongo; udongo wako unaweza kuwa hauna uwezo wa kubeba mzigo wa jengo lako au udongo unamomonyoka kutokana na mtiririko wa maji karibu na msingi wako. Udongo wa kichanga unaweza kuoshwa na maji yanayopita na kusababisha kumomonyoka na kisha kutumbukia chini kwa jengo lako. Pia Maeneo yenye shughuli za uchimbaji yanaweza kukumbwa na matatizo ya udongo kutumbukia chini kisha kuathiri jengo lako. Maeneo yenye udongo wenye chokaa yanaweza kukumbwa na matatizo ya kutumbukia kwa ardhi. Ni muhimu kuweza kufanya ukaguzi katika eneo lako kwa kuangalia nyumba ambazo tayari zimeshajengwa, majengo ya zamani, nyufa na mashimo katika ardhi n.k ili kuweza kufanya tathmini ya namna ya kuuendea ujenzi wako.

Pia inawezekana udongo wako ni mfinyanzi; udongo mfinyanzi una tabia ya kutanuka pindi upatapo maji na kusinyaa pindi maji yakaukapo; hali hii inaweza kusababisha msingi wa nyumba yako kutingishwa na mwisho wa siku ukaleta nyufa. Udongo mfinyanzi unatanuka na kusinyaa; hali hii inaweza kuonekana pia kwa kuvimba na kupasuka kwa paving slabs katika sakafu na nyua, mabomba katika ardhi kupasuka, kubanwa kwa milango na madirisha pamoja na nyufa katika kuta na sakafu. Uwepo wa miti jirani na nyumba yako huweza kuathiri udongo ulio katika nyumba yako katika vipindi vya majira ya mwaka kisha kusababisha nyufa katika nyumba yako; mizizi ya miti pia huweza kusababisha nyufa katika nyumba yako pindi inaposambaa.

Sababu nyingine ambayo inaweza kusababisha nyufa katika msingi ni ujenzi mbovu. Kujenga bila kufuata taratibu za kitaalamu zinazotakiwa katika kusanifu jengo na katika kujenga jengo lako huweza kusababisha ubovu wa msingi wa nyumba yako. Pia utumiaji wa malighafi za ujenzi ambazo zipo chini ya kiwango au kuchakachua malighafi pamoja na kutumia malighafi isivyotakiwa huweza kupelekea msingi wa nyumba yako kuwa mbovu na kupelekea kupata nyufa.

Nyufa katika msingi mara nyingi hupelekea kuta na maeneo ya mengine ya nyumba nayo kupata nyufa na kisha kupelekea nyumba nzima kuwa mbovu. Msingi ndio sehemu ya jengo ambayo hubeba na kulilinda jengo lako salama; ni muhimu kuweza kujenga msingi wako kwa kufuata taratibu za kitaalamu ili kuhakikisha ubora. Pia ni muhimu kuweza kutafuta Wataalamu husika pindi uonapo matatizo ya nyufa katika msingi wako ili kuweza kurekebisha na kuponya nyumba yako iweze kudumu vyema.

Nyufa katika slab

Nyufa katika slab za sakafu mara nyingi hutokea kama sakafu haina uwezo wa kubeba mzigo. Sakafu katika nyumba yako ina kazi mojawapo ya kubeba mzigo wa vitu vinavyokaa juu yake; hivyo kama uzito unaobebwa unazidi uwezo wa sakafu basi kuna uwezekano wa sakafu kupasuka.

Ubovu wa sakafu unaweza kutokea pia kutokana na ujenzi mbovu; kutumia malighafi zilizo chini ya kiwango na za kuchakachuliwa. Ubovu wa sakafu unaweza kutokana na ujenzi mbaya bila kufuata taratibu za kitaalamu zinazotakiwa. Ujenzi mbovu hufanya slab yako kuwa mbovu na kushindwa kuwa na uimara ule unaotakiwa hivyo kushindwa kubeba mzigo.

Nyufa katika slab huweza kutokea pia kama sehemu ambayo sakafu imekaa haipo vyema; kama slab ya ghorofani imekaa katika beams na nguzo ambazo zipo mbovu, basi ubovu wa nguzo, beams na msingi huweza kusababisha hata slab nayo kupata ubovu na kisha kuleta nyufa. Kama ni sakafu iliyo juu ya ardhi, basi kama material yaliyo chini ya sakafu hayajashindiliwa vizuri au kama yanamomonyoka au kama hayapo imara basi huweza kusababisha sakafu nayo kuyumba na kupata nyufa.

Nyufa katika kuta

Nyufa katika kuta huweza kutokea kwa sababu mbalimbali ikiwemo kutitia kwa nyumba, kusinyaa na kutanuka kunakotokana na joto, mitingishiko mbalimbali ambayo inaweza kuikumba nyumba pamoja na kupenya kwa maji na kemikali katika kuta. Nyufa kubwa katika kuta ni hatari na zinaweza kusababisha matatizo mbalimbali ikiwemo wanyama na wadudu hatari kupenya, wezi na hata kuanguka nyumba.

Kutitia kwa nyumba ni kawaida ya jengo lolote ikiwemo kama hatua ya jengo kuweza kutengemaa baada ya kujengwa. Pale kutitia kunapotokea kwa namna ambayo upande mmoja na upande mwingine kutofautiana kiasi cha mtitio, basi jengo lako linakuwa katika hatari ya kupata nyufa. Nyufa ambazo zinaweza kupata jengo lako ni katika msingi na kuta; nyufa katika kuta ni pamoja na zile zinazotoka katika msingi. Kwasababu ya jengo kutokaa katika msawazo, basi mzigo wa jengo unakuwa unalalia upande mmoja, hali hii huweza kusababisha baadhi ya kuta kushindwa kuhimili mzigo huo na baadaye kupelekea nyufa. Nyufa katika kuta ambazo zinatokana na kutitia kwa jengo huweza kuonekana kwa namna ya ngazi ngazi katika kuta na pia kwa mshazari unaoelekea juu kutoka katika kona za milango na madirisha.

Kuwepo na miti jirani na jengo lako kunaweza sababisha kuvimba na kusinyaa kwa ardhi katika vipindi mbalimbali vya mwaka katika udongo wa mfinyanzi. Kuvimba na kusinyaa huku kunaweza sababisha jengo lako kuleta nyufa katika msingi na kuta. Udongo mfinyanzi wenyewe peke yake pia huweza kusababisha jengo lako kutitia katika vipindi mbalimbali vya mwaka kutokana na mabadiliko ya unyevunyevu. Kwa ujumla pale ambapo udongo wa karibu na jengo lako pale unapokuwa haujatulia vyema, huweza kusababisha nyufa mbalimbali katika kuta na jengo kwa ujumla.

Jua linapowakia kuta zako katika vipindi mbalimbali vya mwaka huweza sababisha kulegea kwa kuta kama hazijajengwa katika uimara unaotakiwa. Kusinyaa na kutanuka kwa kuta kunakotokana na joto na baridi kunaweza sababisha kulegea kwa ukuta wako kisha vinyufa vidogovidogo kutokea; vinyufa hivi huweza kukua na kufikia kuwa kubwa. Uimara wa ukuta unatokana na namna ambavyo umejengwa na malighafi ambayo imetumika; ujenzi mbovu na wa kuchakachua huweza kukumbwa na aina hii ya nyufa katika kuta zako. Kuta zilizo jirani na vyanzo vya moto kama vile maeneo ya jikoni, chimney n.k huweza kukumbwa na tatizo hili la nyufa kama ujenzi wake haukufanyika katika viwango vinavyotakiwa.

Kuvuja kwa majimaji na kemikali mbalimbali katika ukuta wako kwaweza sababisha kuvimba kwa ukuta na kupelekea nguvu ya msukumo ndani yake. Ukuta unapolegea mwisho wa siku huweza kuleta nyufa. Maji yanayovuja kutokana na kupasuka kwa mabomba yaliyo ndani ya kuta hutafuta njia ya kutokea kwa msukumo; nguvu msukumo huu hulegeza sehemu iliyo na udhaifu zaidi na kisha kusababisha nyufa katika ukuta wako. Unyevunyevu ulio katika vishimo vidogovidogo vya ukuta wako hupata kutanuka na kisha kuleta ulegevu katika tofali lako na mwishowe kuleta nyufa katika ukuta. Maji yenye chumvi chumvi huweza kuathiri nondo zilizo katika ukuta na kupelekea nondo hizo kupata kutu ambayo nayo huweza kupasua ukuta wako kwa nyufa. Baadhi ya kemikali huweza kuwa na athari katika kuta zako kama zitaweza kuufikia ukuta; kemikali kama tindikali, chumvichumvi, alkali n.k huweza kuleta mabadiliko mbalimbali ya kikemikali na kisha kuuathiri ukuta wako. Kwaujumla, nyufa za namna hii hutokana na ujenzi mbovu pamoja na utumiaji wa malighafi zilizochakachuliwa au zilizo chini ya kiwango.

Mzigo ulio juu ya kuta unaweza kuleta tatizo la nyufa katika kuta kama haujakaa katika hali ya usawa; kuta ambazo zimebeba mzigo juu yake zinatakiwa kuwa na uwezo wa kuhimili uzito huo. Pale ambapo uzito wa mzigo ukashinda uwezo wa ukuta basi, matatizo yanaweza kutokea ikiwemo nyufa au kuanguka kabisa kwa ukuta. Slab ambazo zimekaa juu ya ukuta zinapaswa kuweza kuandaliwa kitaalamu namna ya kukaa juu yake bila kuleta nguvu momenta itakayoushinda ukuta; kama nguvu ya momenta itakuwa kubwa kuliko uwezo wa ukuta basi kuna uwezekano mkubwa wa nyufa kutokea.

Paa la nyumba ambalo limekaa na kufungwa juu ya kuta laweza kuleta madhara ya nyufa katika kuta kama halijaandaliwa vyema inavyotakiwa. Kenchi za paa zinapaswa kukaa juu ya kuta vyema bila kuleta nguvu momenta isiyotakiwa; ufungaji mbaya wa kenchi juu kuta waweza sababisha kubinukia kwa nje kwa kuta (truss spread). Kwa maeneo ambayo kuna upepo mkali, kama paa lako halijaandaliwa na kufungwa vyema ikiwemo na maegemeo yake, basi yaweza sababisha mitikisiko mikubwa ambayo yaweza kupelekea kulegea na nyufa katika kuta zako. Kenchi za chini zaweza kupata unyevu na kupanuka wakati kenchi za juu zipo katika hali ya ukavu zaidi, hali hii yaweza sababisha kulegea kwa paa na kepelekea nguvu msukumo katika kuta ambao waweza sababisha nyufa.

Hatua za msingi za kufanya marekebisho

Namna ya kufanya marekebisho ya nyufa katika nyumba hutegemea zaidi aina ya ufa, kiasi na sehemu ulipo ufa wako. Kitu cha kwanza ni kujua aina hiyo ya ufa unatokana na nini? Sababu iliyopelekea ufa huo kutokea. Hapa inahitajika utaalamu mzuri wa kuweza kujua namna ya kutambua sababu sahihi ambayo imepelekea ufa katika nyumba yako. Pia inatakiwa kujua kiasi cha athari ambacho kimetokea katika ufa wako. Hatua nyingine ni kujua kama ufa wako bado unaendelea kukua au hauendelei tena. Baada ya hapo inatakiwa kuweza kutibu chanzo kabisa cha tatizo lililopelekea ufa huo kutokea ili usiweze kutokea tena. Baada ya hapo inatakiwa kutibu athari ambazo ufa umesababisha ili kuweza kuliweka jengo lako katika hali iliyosawa. Hatua zote hizi zinahitaji utaalamu wa kutosha ili kuweza kutoa tiba sahihi.

Nyufa katika nyumba ni moja ya matatizo ambayo hukumba majengo yetu; waswahili husema “usipoziba ufa, basi utajenga ukuta”; ni vyema kuweza kurekebisha matatizo mbalimbali katika jengo lako ili kuweza kuliongezea uimara na kudumu zaidi. Lakini pia katika ujenzi, ni muhimu kuweza kufuata taratibu zinazopaswa katika ujenzi ili kuweza kuepuka matatizo mbalimbali ambayo yanaweza kutokea siku za mbeleni.

4 responses

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ID-18184
4
265 sqm
182 Pcs
20 m
4,744 Pcs
17 m
2,359 Pcs
ID-17013
2
89 sqm
61 Pcs
12 m
1,593 Pcs
11 m
792 Pcs
ID-16941
3
167 sqm
115 Pcs
15 m
2,989 Pcs
13 m
1,486 Pcs
ID-27544
4
252 sqm
211 Pcs
20 m
4,511 Pcs
16 m
2,243 Pcs
ID-16678
3
150 sqm
135 Pcs
14 m
3,200 Pcs
12 m
1,100 Pcs
ID-27594
3
193 sqm
157 Pcs
16 m
3,455 Pcs
15 m
1,718 Pcs
ID-17754
3
153 sqm
105 Pcs
15 m
2,741 Pcs
12 m
1,363 Pcs
ID-27605
3
185 sqm
152 Pcs
16 m
3,312 Pcs
15 m
1,647 Pcs
ID-20447
4
256 sqm
176 Pcs
20 m
4,573 Pcs
17 m
2,274 Pcs
ID-17204
4
223 sqm
153 Pcs
19 m
4,023 Pcs
17 m
1,985 Pcs
ID-21763
4
232 sqm
160 Pcs
18 m
4,153 Pcs
17 m
2,065 Pcs
ID-21633
4
361 sqm
127 Pcs
16 m
9,917 Pcs
14 m
2,096 Pcs
Makazi Icon Blue

Join Membership

Join Membership to See Clear Floor Plans Before You Buy the Full Plan; See How Much MONEY is Needed to INVEST in Your Business In order to Get the Profit to Finance Construction of This House. What MORTGAGE to Borrow and Return Monthly to Your Bank. Also, See How Much it COSTS to Build the Foundation, Walling, Roofing, Ceiling, Painting, Doors, Windows… in All of Our Houses on This Platform so That You Can CHOOSE, COMPARE, PLAN & STRATEGIES on How to Approach Your Construction Rightly!