Nini uhalisia wa nyumba ndogo?
Tunapokuja katika swala la ujenzi wa makazi ya kuishi familia, basi kuna mambo amabyo yamekuwa kama sheria ambayo yanaamua aina ya nyumba ambazo tunajenga. Baadhi ya mambo ni kama bajeti, tamaduni, majirani, hali ya hewa, staili… Kiujumla ktk jamii yetu tunapozungumzia nyumba ndogo tunamaanisha ni zile nyumba ambazo zinatumia nafasi ndogo ya kiwanja, zinazotumia bajeti ndogo, zilizo na urahisi kujenga n.k. Nyumba ndogo mara nyingi ni zile nyumba ambazo ukubwa wa sakafu wake upo chini ya mita za mraba 100 (sqm) na mara nyingi ni nyumba za vyumba 3 au viwili za kawaida (siyo ghorofa).
Hivyo kitaalamu nyumba ndogo ni zile nyumba ambazo zipo chini ya mita za mraba ~100 na zenye unafuu na urahisi kujenga. Maana hii inaweza badilika kutokana na mtu binafsi ambavyo anaweza kuamua. Maana hii pia inaangalizia zaidi jamii ya Kitanzania na Afrika Mashariki, hivyo kwa mtu ambaye yupo Ulaya anaweza kuta maana hii haikidhi sana.
Gharama za kujenga nyumba ndogo
Je, gharama za ujenzi za nyumba ndogo ni kiasi gani? Hili ni swali ambalo umekuwa ukihitaji kujibiwa. Kikawaida nyumba ya vyumba vitatu ya kawaida yenye ukubwa wa sakafu wa 120sqm kujenga Tanzania mpaka kuikamilisha finishing vyema ktk ubora mzuri itagharimu Tshs. ~50 – 65 Milioni, sasa tunapokuja nyumba ndogo inaweza gharimu kuanzia Tshs. 25 – 45 Milioni. Gharama hizi zinategemea sana na ukubwa haswa wa nyumba husika, staili na mtindo wa nyumba, idadi ya vyumba ktk jengo. Kujenga boma (msingi, kuta na paa) kwa nyumba hizi zinaweza kukugharimu kiasi cha Tshs. ~10 – 25 Mil kutegemeana na nyumba. Kwa Yule anayehitaji kujua gharama halisi kila nyumba ktk ramani zetu basi jiunge uanachama hapa ili uweze ona gharama kwa kila hatua ujenzi (msingi, kuta, paa, sakafu, dari, umeme…).
Sababu za watu kujenga nyumba ndogo
Zipo sababu nyingi ambazo zinaamua watu kujenga nyumba hizi ndogo na sasa tutaziangalia ili nawe uweze jihakiki kama kweli unahitaji kujenga nyumba hizi au huhitaji. Tutaangalizia pia na faida na hasara za kujenga nyumba ndogo.
- Kuwa na bajeti ndogo kujenga
Watu wengi siku hizi wamekuwa wanataka kujenga nyumba ambazo zimejitoshereza kiuzuri lkn pia wataweza mudu gharama za ujenzi. Kutokana na kuwa na kiasi kidogo cha bajeti basi watu wengi wamekuwa wakiamua kujenga nyumba ambazo watamudu gharama lkn pia watazikamilisha vyema. Je, una Tshs. 15M na unataka kufanya ujenzi mzuri uliokamilika? Ndio inawezekana kwa kuanzia pesa hiyo kukamilisha boma la nyumba yako na ukahamia. Ijapokuwa pia ukijikita tuu kwenye gharama ndogo unaweza jikuta unaibana nyumba ikawa ndogo na ukapunguza uzuri, hivyo ni muhimu kubalance vyema bajeti na mahitaji yako. Fahamu zaidi gharama za ujenzi wa nyumba na namna ya kuokoa gharama ujenzi.
- Eneo dogo la kiwanja
Viwanja ni gharama kununua haswa vile ambavyo vipo ktk maeneo muhimu na mazuri. Hivyo kama kiwanja chako ni kidogo na unapenda ujenge hapo basi unaweza jenga nyumba hizi ndogo vyema kabisa. Ni muhimu pia kuwa na uhalisia kama kiasi cha kiwanja hicho kitaweza kukutoshereza kwa shughuli zako zote unazotarajia ili uweze furahia nafasi yako. Fahamu zaidi aina ya kiwanja kinachofaa kununua.
- Familia ya watu wachache
Zipo baadhi ya familia ambazo idadi ya watumiaji wa nyumba ni 3 tuu. Kuna wazee ambao wamestaafu, pia wale ambao wameamua kuishi bila kuoa aua kuolewa na labda wageni ambao unakuta wanataka nyumba ya kutosha watu wachache ambapo wanajikuta nyumba ambazo zinawafaa ni hizi za ramani ndogo. Hapa pia ni muhimu kuangalia kama idadi inaweza ongezeka au laa siku za mbeleni na kama nyumba itatosha.
- Nyumba za kupangisha
Nyumba za kupangisha ni biashara nzuri na endelevu maana inakuletea kipato endelevu mara kwa mara kwa muda mrefu. Nyumba ya kupangisha ni uwekezaji hivyo inabidi ilete faida kwa muda wa haraka iwezekanavyo; Hivyo ni muhimu kujenga nyumba ya kupangisha ya vyumba 3 au 2 ndogo iliyojitoshereza na kutumia gharama ndogo kiujenzi ili kodi ambayo wateja watakuwa wanakulipa iweze rudisha haraka gharama yako ya ujenzi. Mtu aliyejenga nyumba kwa 30M atarudisha haraka gharama yake kuliko yule aliyetumia 50M na unaweza kuta kiasi cha pango kipo sawa. Ijapokuwa pia ni vizuri kuangalia ni aina ipi ya wateja wako unataka kuwapangisha ktk nyumba yako; je, ni wanaopenda nyumba kubwa au wanatosheka hata kwa nyumba ndogo?
- Gharama ndogo za uendeshaji
Gharama za nyumba hazipo tuu ktk ujenzi, zipo pia ktk uendeshaji. Tunapozungumzia uendeshaji tunamaanisha kulipia gharama za usafi, matengenezo, kodi za serikali, umeme, maji, taka n.k. Hivyo kuna mwingine anataka gharama zake za kuendesha nyumba ziwe ndogo zaidi kwa kuchagua kujenga nyumba ndogo.
Orodha ya ramani za nyumba ndogo
Sasa hapa chini tumekupa ramani za nyumba ndogo ambazo zinafaa kujenga kwa anayehitaji kujenga nyumba ndogo na akafurahia. Ni nyumba ambazo zimeandaliwa kuangalia mazingira yetu kiuhalisia na kufuata viwango vitakavyokupa ladha nzuri ya kuzitumia.
Ramani ID-11210, vyumba 3, tofali 1096+418 na bati 50
- vyumba 3 (1 kina bafu ndani), sebure dining jiko stoo, choo public, veranda 2
- gharama ya kujenga boma (msingi, kuta na bati) = Tshs~13 Mil
- kiwanja kisipungue = 14x15m
- ukubwa = 67sqm
Ramani ID-7780, vyumba 3, tofali 1146+860 na bati 60
Nyumba hii imeandaliwa ili iwe simple lkn pia itumie nafasi kidogo ya kiwanja chako. Staili yake ya bati haitumii bati nyingi hivyo utaweza okoa gharama ktk vifaa pia. Nyumba hii inaweza faa zaidi maeneo ya joto sababu jiko na dining vipo ktk baeaza lililo wazi. HAitumii nguzo za zege sana hivyo utaokoa gharama za zege.
- vyumba 3 (1 kina bafu ndani), sebure dining jiko stoo, choo public, veranda 2
- gharama ya kujenga boma (msingi, kuta na bati) = Tshs~18 Mil
- kiwanja kisipungue = 13x16m
- ukubwa = 77sqm
Ramani ID-7823, vyumba 3, tofali 1200+645 na bati 65
Nyumba hii ipo zaidi kwa ukatikati kwa maana unaweza iona kama ipo kawaida lkn ina unafuu. Nyumba hii ina vyumba 3 vya kulala na sebure jiko dining na choo ndani; veranda zake zimetengenezwa kwa tofali ili usitumie zege sana na pia nyumba yote imepigwa bati hivyo utaokoa gharama sana.
- vyumba 3 (1 kina bafu ndani), sebure dining jiko stoo, choo public, veranda 2
- gharama ya kujenga boma (msingi, kuta na bati) = Tshs~23 Mil
- kiwanja kisipungue = 14x17m
- ukubwa = 99sqm
Ramani ID-7786, vyumba 3, tofali 830+553 na bati 62
Kijumba hiki kina ladha ya kipekee na watu wengi wamekichukua kwajili ya kujenga. Rangi na staili yake ya paa, kuta na madirisha zinawavuta wengi kujenga. Okey, ukubwa wa madirisha unaongeza gharama ujenzi lkn tumeweka hivyo ili kuleta mvuto wa nyumba. Nyumba hii inafaa kwa yule ambaye usafi kwake sio shida. Kumbuka kutumia fundi mzuri ktk kujenga nyumba hii ili uweze ifurahia mwonekano wake
- vyumba 3 (1 kina bafu ndani), sebure dining jiko stoo, choo public, veranda 2
- gharama ya kujenga boma (msingi, kuta na bati) = Tshs~26 Mil
- kiwanja kisipungue = 14x17m
- ukubwa = 99sqm
Ramani ID-7790, vyumba 3, tofali 1480+798 na bati 65
Jenga nyumba hii kama unahitaji ukawaida lkn ulio na unafuu ki gharama; hapa namaanisha mpangilio wa vyumba kidogo upo kikawaida lkn umebana kiasi fulani. Nyumba hii inakupa nafasi tofauti ya choo na bafu bvya public hivyo ukaweza nufaika na muingiliano wa vyumba hivyo kishughuli.
- vyumba 3 (1 kina bafu ndani), sebure dining jiko stoo, choo public, veranda 2
- gharama ya kujenga boma (msingi, kuta na bati) = Tshs~22 Mil
- kiwanja kisipungue = 14x17m
- ukubwa = 90sqm
Ramani ID-7851, vyumba 3, tofali 1936+1088 na bati 80
Nyumba hii ina ukubwa kiasi fulani lkn bado inaangukia ktk kundi la nyumba ndogo. Ni vyumba 3 ambayo unaweza ijenga na ukaokoa gharama na nafasi ya kiwanja chako vyema. Staili la paa lake ni la kipekee na utahitaji fundi mzuri kuijenge.
- vyumba 3 (1 kina bafu ndani), sebure, dining jiko stoo, choo public, veranda 2
- gharama ya kujenga boma (msingi, kuta na bati) = Tshs~24 Mil
- kiwanja kisipungue = 17x17m
- ukubwa = 103sqm
Ramani ID-17013, vyumba 2, tofali 1593+792 na bati 61
Hiki kijumba cha vyumba 2 ni kizuri sana na kinavuta sana kimuonekano. Ni nyumba ambayo inavyumba 2 vya kulala ambapo kimoja ni master na kingine cha kawaida. Ijenge na uweze furahia mwonekano na ladha nzuri.
- vyumba 2 (1 kina bafu ndani), sebure dining, jiko stoo, choo public, veranda 2
- gharama ya kujenga boma (msingi, kuta na bati) = Tshs~21 Mil
- kiwanja kisipungue = 15x16m
- ukubwa = 89sqm
Ramani ID-11264, chumba 1, tofali 698+313 na bati 32
Kijumba hiki cha chumba kimoja kinafaa sana kwa yule anayependa staili simple. Unapata chumba kimoja kilicho na ukubwa wa kawaida ambapo choo utatumia cha public ambacho nacho kimekaa jirani na chumba.
- vyumba 1, sebure dining jiko stoo, choo public, veranda 1
- gharama ya kujenga boma (msingi, kuta na bati) = Tshs~6 Mil
- kiwanja kisipungue = 11x12m
- ukubwa = 32sqm
Ramani ID-13471, vyumba 2, tofali 1389+514 na bati 61
Nyumba hii ya vyumba 2 ni special kwa yule ambaye anapenda kubarizi nje; jiko na dining vipo nje ktk veranda hivyo utakuwa unapata upepo mwanana. Ni nzuri kwa yule ambaye anajenga nyumba ktk maeneo ya joto.
- vyumba 2 (1 kina bafu ndani), sebure, dining jiko stoo, choo public, veranda 1
- gharama ya kujenga boma (msingi, kuta na bati) = Tshs~17 Mil
- kiwanja kisipungue = 13x15m
- ukubwa = 72sqm
Ramani ID-17760, vyumba 2, tofali 1217+605 na bati 47
Nyumba ya vyumba viwili ya staili na rangi ya namna fulani. Ina sebure ambayo hapohapo unaweza tumia kwajili ya shughuli nyingine kama kupikia dining na kuhifadhi vitu. Waweza tumia kijinafasi ktk korido kuhifadhia vitu au kutumia kwa shughuli nyingine ambayo haita maliza nafasi yako.
- vyumba 2 (1 kina bafu ndani), sebure dining jiko stoo, choo public, veranda 1
- gharama ya kujenga boma (msingi, kuta na bati) = Tshs~16 Mil
- kiwanja kisipungue = 13x14m
- ukubwa = 68sqm
Ramani ID-17004, vyumba 3, tofali 1705+846 na bati 65
Nyumba nzuri ya kipekee ya vyumba 3 ambapo chumba kimoja kina choo ndani. Ina sebure na dining vilivyo ktk sehemu moja, pia zina jiko na stoo vilivyo ktk eneo moja ila kwa kujitoshereza. Jenga nyumba hii na ufurahie rangi nzuri na mwonekano wa nyumba yako.
- vyumba 3 (1 kina bafu ndani), sebure dining, jiko stoo, choo public, veranda 2
- gharama ya kujenga boma (msingi, kuta na bati) = Tshs~22 Mil
- kiwanja kisipungue = 13x16m
- ukubwa = 95sqm
Ramani ID-10129, vyumba 3, tofali 2024+890 na bati 33
Staili hii ya nyumba ambayo bati halionekani inaitwa contemporarty style; Nyumba hii ni ya vyumba 3 ambapo kimoja kina choo ndani. Ni nyumba kali na yenye hisia za kitofaiti ambapo utaweza ifurahia ktk kuitumia na watu wataipenda kuiona. Tumia fundi ambaye byupo vizuri sana ili uweze iona ktk uhalisia wake.
- vyumba 3 (1 kina bafu ndani), sebure dining jiko stoo, choo public, veranda 2
- gharama ya kujenga boma (msingi, kuta na bati) = Tshs~30 Mil
- kiwanja kisipungue = 15x17m
- ukubwa =100sqm
Ramani ID-17614, vyumba 2, tofali 1369+681 na bati 53
Nyumba hii ni ya kinamna nzuri ambapo mpangilio wa vyumba vyake ndani umepangiliwa vyema na utaweza ufurahia. Ina vyumba viwili na chumba kimoja kina choo ndani. Tumia fundi mzuri kuijenga ili fundi aweze itendea haki ktk staili na mwonekano.
- vyumba 3 (1 kina bafu ndani), sebure dining jiko stoo, choo public, veranda 2
- gharama ya kujenga boma (msingi, kuta na bati) = Tshs~18 Mil
- kiwanja kisipungue = 13x14m
- ukubwa =76.5sqm
Ramani ID-11258, vyumba 2, tofali 780+414 na bati 45
Nyumba safi ya vyumba 2 ambapo kila chumba ni cha kawaida. Ina sebure dining jiko stoo na veranda ya mbele pamoja na choo kimoja cha pamoja. Ipo simple kama ilivyo na pia ipo na gharama simple sana kuliko nyumba nyingi.
- vyumba 2, sebure dining jiko stoo, choo public, veranda 1
- gharama ya kujenga boma (msingi, kuta na bati) = Tshs~9 Mil
- kiwanja kisipungue = 12x14m
- ukubwa =50sqm
Ramani ID-22351, vyumba 2, tofali 780+414 na bati 45
Nyumba safi ya vyumba 2 ambapo kila chumba ni cha kawaida. Ina sebure dining jiko stoo na veranda ya mbele pamoja na choo kimoja cha pamoja. Imeongezewa mwonekano fulani wa kiurembo ili kuvutia zaidi bila kubadili unafuu wake sana.
- vyumba 2, sebure dining jiko stoo, choo public, veranda 1
- gharama ya kujenga boma (msingi, kuta na bati) = Tshs~11 Mil
- kiwanja kisipungue = 12x14m
- ukubwa =48sqm
Ramani ID-17746, vyumba 2, tofali 1522+757 na bati 58
Nyumba safi na kipekee ya vyumba 2 ambapo chumba kimoja kina choo ndani na kimoja cha kawaida. Inajengwa kwa kutumia tofali za kuchoma (waweza pia tumia tofali za cement-block au interlocking blocks). Furahia maisha mazuri na familia yako huku ukipata raha ya uhalisia wa maisha.
- vyumba 2, sebure dining, jiko stoo, choo public, veranda 2
- gharama ya kujenga boma (msingi, kuta na bati) = Tshs~20 Mil
- kiwanja kisipungue = 13x15m
- ukubwa =85sqm
Ramani ID-15831, vyumba 1, tofali 931+463 na bati 27
Staili ya kipekee ya nyumba ambapo hapo unapata nyumba ya chumba kimoja chenye jiko na sebure. Ni nyumba ambayo imeangalia zaidi mwonekano na staili ili kukupa ladha inayofaa. Ijengee kwa kutumia fundi mzuri ili uweze ifurahia kimwonekano na staili yake original.
- chumba 1, sebure dining, jiko stoo, choo public, veranda 1
- gharama ya kujenga boma (msingi, kuta na bati) = Tshs~15 Mil
- kiwanja kisipungue = 13x13m
- ukubwa =52sqm
Mambo ya muhimu unapotaka kujenga nyumba ndogo
Unapotaka kujenga nyumba ndogo ni muhimu kwanza ujijengee msimamo wa kuwa utaijenga nyumba hiyo katika ubora na taratibu zinazofaa bila kuchakachua kiwango cha ubora na uzuri. Ni muhimu kujenga nyumba ile ambayo unaona utaweza imudu kwa kiasi cha muda ambao umepanga kuijenga. Kumbuka kutumia wataalamu husika ikiwamo kutumia ramani kamili zenye ubora kama hizi za nyumba gharama ndogo tulizo zionesha hapa pamoja na mafundi walio na kiwango kizuri. Kumbuka kuwa nyumba ndogo haimaanishi ubora mbaya wa nyumba; unaweza jenga nyumba nzuri na ikawa nzuri na ya kuvutia sana kuliko yule aliyejenga ghorofa kwa kuchakachua.
Je, katika nyumba hizo tulizo ziorodhesha hapo juu, ni ipi ambayo inakufaa na umeipenda zaidi?
5 responses
Kazi nzuri
Kazi nzuri
napaje Ramani ya nyumba ya vyumba viwili.
where is your location for further discussions?
Good work