Tunjenga nyumba aina ya contemporary roof au nyumba zilizofichwa paa popote pale katika mikoa yote ya Tanzania. Tunafika na kujenga pamoja na nje ya nchi katika maeneo ya Afrika Mashariki, Zambia, Malawi na nchi nyingine zinazozunguka Tanzania. Tunatumia mfumo wetu wa ujenzi na kujenga kulingana na ramani ambayo utatupatia. Pia, sisi wenyewe tuna utaalamu mzuri kuhusiana na mambo ya ujenzi.
TUNAYOZINGATIA KTK UJENZI WA CONTEMPORARY ISIVUJE
– Mifereji na Maji ya Mvua: Tunahakikisha mifereji ni mikubwa na imara, tunatumia gata kubwa na downpipes idadi ya kutosha kwa ajili ya kutoa maji ya mvua haraka na kwa usahihi.
– Ulalo Sahihi wa Paa: Tunazingatia ulalo wa bati kuhakikisha uko ndani ya kiwango kinachohitajika ili kuepuka backflow ya maji, na ulalo sahihi wa paa unahakikisha maji yanapita vizuri na hayatuami juu ya bati.
– Kupigaji Sahihi wa Bati: Tunatumia misumari sahihi na kupiga kwa njia sahihi ili kuhakikisha bati zimewekwa vizuri na kwa usalama, na tunajitahidi kutumia bati ndefu zisizo za kuunga unga ili kuepuka maeneo ya kuvuja.
– Uwekaji wa Vichujio: Tunaweka vichujio kwenye downpipes juu ili kuzuia takataka kuziba downpipes; vichujio vinawekwa kwa namna ambayo maji yanaweza kupita kwa urahisi lakini takataka zinazuiwa.
– Waterproofing: Tunafanya waterproofing kwenye maungio ya bati na kuta au zege inapohitajika ili kuzuia uvujaji, na waterproofing inafanywa kwa kutumia vifaa na mbinu za kisasa kuhakikisha uimara wa paa.
HUDUMA TUNAZOTOA:
1. Huduma Kamili za Ujenzi:
– Tunahusika na mchakato mzima wa ujenzi kuanzia msingi hadi kumalizia.
– Tunajenga kulingana na viwango vya kitaalamu na kufuata sheria husika.
– Tunahusika kujenga kwa hatua mbalimbali za ujenzi kulingana na mteja atakavyochagua kwa steji kama:
– – Msingi
– – Kuta
– – Zege
– – Paa
– – Madirisha
– – Milango
– – Sakafu
– – Dari
– – Rangi
– – Mashimo ya Vyoo
– – Mabomba
– – Umeme
– – Mandhari
2. Mchakato wa Ujenzi:
– Tunaweza kujenga nyumba kulingana na mfumo utakubaliana na mteja.
– Tunaweza kujenga nyumba zote kwa pamoja au kwa awamu kulingana na bajeti yako.
– Mteja anaweza kununua na kuhifadhi vifaa mwenyewe.
3. Muda na Gharama:
– Tunaweza kumaliza ujenzi wa nyumba yako ndani ya miezi miwili.
– Tunahakikisha kwamba nyumba yako inajengwa vizuri na kwa viwango bora.
MAMBO YA KUHAKIKISHA UNAYAJUA KABLA YA KUJENGA NASI:
1. Ramani na vibali:
– Hakikisha una ramani ya kitaalamu na vibali vya ujenzi.
– Tunaweza kukusaidia kuandaa na kupatia vifaa vinavyohitajika.
2. Ununuzi na usimamizi wa vifaa:
– Mteja anawajibika kusimamia ununuzi na utunzaji wa vifaa.
– Hakikisha vifaa vinapatikana karibu na eneo la ujenzi.
3. Ukaguzi na mabadiliko:
– Mteja anapaswa kukagua kazi kila hatua kuhakikisha inafanyika kulingana na mahitaji.
– Tutajadili mabadiliko yoyote ya kazi ili kuhakikisha jengo linakidhi mahitaji yako.
Other Services from House Building Categories
You May Like Again
Cancellation:
Return / Exchange:
Other Profesionals
Join our membership to become a part of our expansive platform dedicated to residential development in Africa. Gain access to house plans, informative articles, vetted builders, plot listings and construction materials!