Orodha ya ramani za nyumba zinazofaa kujengea nyumba ndogo Tanzania
Nini uhalisia wa nyumba ndogo? Tunapokuja katika swala la ujenzi wa makazi ya kuishi familia, basi kuna mambo amabyo yamekuwa kama sheria ambayo yanaamua aina ya nyumba ambazo tunajenga. Baadhi ya mambo ni kama bajeti, tamaduni, majirani, hali ya hewa, staili… Kiujumla ktk jamii yetu tunapozungumzia nyumba ndogo tunamaanisha ni zile nyumba ambazo zinatumia nafasi […]
Fahamu zaidi unapotaka kujenga nyumba bati zisizoonekana (Contemporary houses za Kitanzania)
CONTEMPOARY HOUSES nini? – Contemporary maana yake ni MODERN. Hivyo hizi ni nyumba za kisasa zaidi (zinazo-trend) – Zinasifa za kuwa simple, smart, minimalistic, clear. Zina sura bapa(planes), box style, nyuzi pembe nne, straightness, rangi chache zaidi nyeupe na gray, open space, less privacy as freedom, madirisha na milango mikubwa – Zinatabia ya kutumia vifaa […]
Kazi ya linta katika jengo
Linta ni moja ya kiungo katika jengo ambacho huwekwa juu ya sehemu zilizo achwa wazi katika kuta za jengo ili kubeba mzigo juu yake na kuupeleka salama mpaka katika maegemeo; ni kiungo kinachowekwa juu ya uwazi wa madirisha, milango, mageti n.k ili kuweza kubeba mzigo juu yake bila kunepa. Kiungo hiki ni muhimu kwani uwazi […]
Kazi ya msingi katika nyumba
Msingi ni sehemu muhimu ya jengo ambayo huunganisha jengo na ardhi husika pamoja na kupeleka mzigo wa jengo kwa usalama kabisa katika ardhi. Pasipo msingi, jengo linakuwa halijakamilika na halipo salama. Kikawaida msingi hutumia gharama kubwa katika kujenga ukilinganisha na baadhi ya maeneo katika jengo, gharama hii kubwa inaashiria umuhimu na ulazima wa sehemu hii ya jengo.
TATIZO LA NYUFA KATIKA NYUMBA YAKO
Kuna sababu nyingi za nyufa katika nyumba zetu za makazi; kwa ujumla vinyufa vyembamba katika kuta, dari, lipu n.k inaweza kuwa ni alama ya kusinyaa na kutanuka kwa sehemu mbalimbali katika nyumba yako ambako kwaweza kuwa kunasababishwa na unyevunyevu, joto, mabadiliko ya kikemikali katika vifaa vilivyotumika kujengea nyumba (rangi, maji, cement, nondo…) ambayo husababisha kusinyaa […]
MAANA YA SEBULE – INAPASWA IWEJE?
Sebule kwa kawaida ni sehemu ya ndani ya nyumba ambayo ni maalumu kwa kupumzikia, kujumuika na kupokelea wageni. Kuna muingiliano wa maneno haya living room – sitting room – lounge – lounge room – front room kutegemea na eneo na mabadiliko ya kitamaduni. Maana ya sebule mimi binafsi nimeiona ipo katika KUPUMZIKA, KUJUMUIKA na KUPOKEA […]
UDHIBITI WA TAKA KATIKA NYUMBA NA MIFUMO YAKE
Tuzungumze kuhusu swala zima la kudhibiti taka katika nyumba zetu za kuishi bila kujali ni ya kwako au ni ya kupanga. Kwanza, maana ya takataka ni kitu au vitu ambavyo havifai tena, havitumiki tena, si vya muhimu tena. Japo hiyo tafsiri haijakamilika vizuri. Tafsiri nyingine inasema kwamba, takataka ni vitu ambavyo kwa muda huo si […]
UMUHIMU WA KUTENGENEZA MANDHARI YA NJE YA NYUMBA
Utengenezaji wa mandhari (Landscaping) ni utengenezaji wa mazingira yanayozunguka majengo na makazi ya binadamu ili yawe yenye kukidhi matumizi na yenye kuleta uzuri, mvuto, afya na ustawi wa jamii huku yakizingatia uhifadhi wa mazingira. Utengenezaji huu huusisha kubadili na kuboresha sura na kontua za ardhi, uboreshaji miti na mimea, kuweka vitu na samani katika mandhari […]
MAMBO AMBAYO WANAWAKE HUYAJALI NA AMBAYO HAWAYAJALI SANA KATIKA UJENZI WA NYUMBA
Katika miaka kadha ambapo nimekuwa nikiandaa miradi mbalimbali ya ujenzi wa nyumba za kuishi, moja ya vitu ambavyo nimevigundua ni nafasi ya mwanamke katika ujenzi wa nyumba. Wanawake wamekuwa na mtizamo na mapendeleo tofauti katika ujenzi wa nyumba tofauti na wanaume. Katika familia ambayo kuna mume na mke, utofauti ni rahisi sana kuonekana katika mitazamo […]
FANYA HIVI KUPUNGUZA GHARAMA ZA UJENZI
Moja ya mambo ambayo yamekuwa yakishughulisha na kufikilisha akili za watu wengi ni swala la ujenzi. Jambo ambalo haswa limekuwa lenye kusababisha hiyo tafakari kubwa ni namna ya kuweza kufanikisha gharama zinazohitajika. Gharama ni jumla ya nguvu, rasilimali na uwezo ambao unahitajika ili uweze kupata kitu ambacho unakitaka. Katika ujenzi, gharama huangukia katika rasilimali […]
JE, NI AINA GANI YA NYUMBA INAYOKUFAA KUJENGA?
Swala la ujenzi ni moja kati ya maswala nyeti ambayo yanayowafikirisha watu, taasisi na serikali namna ya kutekeleza. Kiasi kikubwa cha fedha hulipwa ili kuendesha ujenzi. Asilimia kubwa ya uwekezaji kwa watu na taasisiunalenga katika ujenzi. Hata serikali hutumia asilimia kubwa ya bajeti katika ujenzi. Serikali, taasisi, makanisa huwekeza katika ujenzi kwa gharama kubwa. […]
JE, NI AINA GANI YA KIWANJA KINAFAA KUNUNUA?
TAMBUA MAHITAJI YAKO Ni jambo la msingi kwanza kutambua unanunua ardhi kwajili ya kufanyia shughuli gani; je, ni makazi, biashara, huduma za jamii, viwanda n.k. Hii ni hatua ya awali kabisa kwani itakusaidia kuweza kuamua majibu ya maswali mbalimbali utakayo kutana nayo mbeleni. Ni muhimu kuchanganua uhitaji wako wa ardhi katika matumizi utakayofanyia, mipango ya […]